HATIMAYE waimbaji wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab
kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali leo Oktoba 22
ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala.
Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha
Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka
kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.
Bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi
Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.
Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu
kuwa baada ya majigambo mengi kutoka kila pande, leo mzizi wa fitna utakatwa
ndani ya Dar Live.
Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali
kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo
kamwe Isha hawezi kuyagoka.
Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na
kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.

0 Comments