Jokate
Mwegelo akiwasili katika shule ya Sekondari ya Majani Ya Chai ya Vingunguti.
Kulia kwake ni Mkuu wa shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.
Jokate Mwegelo
akitoa hotuba yake katika Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne ya Shule ya secondari ya Majani ya Chai. Katika
Hotuba yake, Jokate alitoa ahadi ya kuwajengea uwanja wa michezo na matundu ya
Vyoo shuleni hapo. Ujenzi huo utaanza baadaye.
Mkuu wa
Shule ya ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kasango Pascal Ngozi akitoa neno la
shukrani baada ya ahadi ya Jokate Mwegelo wa kujenga uwanja wa michezo na
matundu ya vyoo.
Jokate Mwegelo
akimkimkabidhi zawadi ya kuwa mwanamichezo bora wa wanafunzi wa kidato cha nne
wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane
ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango
Pascal Ngozi.
Jokate
Mwegelo akimkimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye nidhamu bora kwa kidato cha nne
wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane
ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango
Pascal Ngozi.
Jokate
Mwegelo akiserebuka na wanamuziki wa bongo fleva wanaosoma katika shule ya
sekondari ya Majani ya Chai wakati wa Mahafali ya Nane yaliyofanyika
juzi. Jokate ameahidi kuijengea shule hiyo uwanja wa michezo na matundu ya
vyoo.
.................................................................................................................
Na Mwandishi
wetu
Mrembo
mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia
jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” ameahidi kujenga uwanja wa
michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini.
Akizungumza katika
Mahafali ya Nane ya shule hiyo, Jokate alisema kuwa ameguswa na changamoto mbalimbali
zinazo ikabili shule hiyo na kuamua
kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.
Tayari
Jokate amekabidhi viwanja vya netiboli na mpira wa kikapu kwa shule ya Sekondari
ya Wasichana wa Jangwani.
Jokate
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, alisema kuwa serikali peke
yake haitaweza kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu na
nyinginezo na hivyo inahitaji msaada kutoka kwa sekta binafasi na wadau.
“Nashukuru
kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi katika mahafali haya, hii imenipa faraja kubwa
sana, nimesikia changamoto mbalimbali, kwa kuanzia nitaanza kujenga uwanja wa
michezo na matundu ya vyoo,” alisema Jokate.
Alisema kuwa
ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo
nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa
nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya
elimu hapa nchini.
Mkuu wa
Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi alisema kuwa wanalazimika kutumia viwanja vya
shule jirani katika kufanikisha masuala ya michezo ambayo ni moja ya masomo
muhimu sana.
Ngozi
alisema kuwa wanatambua kuwa kuna vipaji kibao vya michezo katika shule yao,
lakini kutokana na kukosa viwanja bora wameshindwa kuvitambua.
“Tunashukuru
Jokate kwa ahadi ya kutujengea uwanja wa michezo na matundu ya vyoo, hii itatoa
hamasa kwa wanafunzi wenye vipaji katika michezo mbalimbali kutambuliwa na vile
vile kuendelezwa, bado tuna tatizo la jengo la utawala, samani za ofisini na
kumalizia uzio wa shule, tunawaomba wadau watusaidie kufanikisha hayo,” alisema
Kasango.
Mahafali
hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa bongo fleva, singeli, ngoma
kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kati ya wanafunzi zaidi ya 290 wanaomaliza
kidato cha nne, Kkhalid Ibrahim alitwaa tuzo ya mwanamichezo bora huku Latifa Kihiyo
akitwaa tuzo ya mwanafunzi mwenye nidhamu.






0 Comments