Random Posts

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI THOBIAS ANDENGENYE AFANYA ZIARA CLOUDS MEDIA GROUP NA KUKUTANA NA MKURUGENZI WA VYOMBO HIVYO VYA HABARI NDUGU RUGE MUTAHABA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye kulia akiongea na Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba alipotembelea ofisi za Clouds Media jana jioni, Mkurugenzi aliahidi kutatua changamoto ya utoaji wa elimu kwa umma ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto inayolikabili Jeshi hilo. 

(PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye katikati akipata maelezo ya jinsi wanavyoendesha kipindi cha Jahazi kutoka kwa Mtangazaji Ephraim Kibonde alipotembelea studio za Clouds FM jana jioni 19/10/2016.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye watatu kutoka kushoto, akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Clouds Media bwana Ruge Mutahaba na Watangazaji wa kipindi cha Jahazi alipotembelea ofisi za Clouds Media jana jioni tarehe 19/10/2016. 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiagana na Afisa Mahusiano wa Clouds Media bwana Simon Semalenga kwenye kuhitimisha ziara yake. 

Post a Comment

0 Comments