Random Posts

KINDA WA NIGERIA AIOKOA MAN CITY KUFA NYUMBANI DHIDI YA SOUTHAMPTON EPL.

_91103006_kelechi_iheanacho_getty

Mshambuliaji kinda wa Nigeria Kelechi Iheanacho ameiokoa timu yake ya Manchester City kudhalilishwa nyumbani na Southampton baada ya kuchomoa bao la kusawaisha na kuwa 1-1 dakika 90 mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza mechi iliyopigwa kwenye dimba la Etihadi.

Southampton walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Nathan Redmond dakika ya 27 kutokana na kujichanganya kwa mabeki wa Man City hadi mapumziko wageni walikuwa mbele.

Kipindi cha pili Man City walifanya mabadiliko kwa kumtoa Kevin De Bruyne na nafasi yake kuchukuliwa na Kelechi Iheanacho na mnamo dakika ya 55 Iheanacho aliisawazishia Man City akipokea pasi nzuri ya Leroy Sane.

Timu Man City walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Vicent Kompany na Leroy Sana na nafasi zao kuchukuliwa na Jesus Navas na Nolito wakati Southampton waliwatoa Jordy Clasie,Dusan Tadic na Charlie Austin na kuwaingiza Ward Prowse,Sofiane Boufal na Pierre Hojbjerg hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuzisaidia timu zao.

Kwa matokeo hayo Man City wanapanda hadi nafasi yao ya kwanza wakiwa na pointi 20 sawa na timu za Arsenal na Liverpool ila wao wakiwa na uwiano mzuri wa kufanga na kufungwa.

VIKOSI:

Manchester City (3-5-1-1):
Bravo 6; Stones 5, Kompany 6 (Navas 78), Kolarov 6; Sane 7 (Nolito 90), Gundogan 6, Fernandinho 6, De Bruyne 5.5 (Iheanacho 46, 7), Sterling 6; Silva 6; Aguero 6
Subs not used: Caballero, Reges, Clichy, Otamendi
Booked: Kolarov, Kompany, Aguero
Goal: Iheanacho 55
Manager: Pep Guardiola 6 
Southampton (4-2-3-1):
Forster 7; Martina 7.5, Van Dijk 8, Fonte 7, McQueen 7.5; Clasie 6.5 (Hojbjerg 67, 6), Romeu 7; Davis 6, Tadic 6 (Boufal 70, 6), Redmond 7; Austin 6 (Ward-Prowse 83)
Subs not used: McCarthy, Yoshida, Rodriguez, Stephens
Booked: Clasie, Romeu, Forster
Goal: Redmond 27
Manager: Claude Puel 7 
Referee: Mark Clattenburg 6
Star man: Van Dijk
*Player ratings by Kieran Gill