Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu Bw. Dotto James (kulia) wakiandika pointi muhimu wakati Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim, alipowahutubia Mawaziri wa Fedha na Makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi za Kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC-Marekani.
Wajumbe
wa Tanzania waliohudhuria mkutano wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha
Duniani-IMF, wakimsikiliza kwa makini Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (hayupo
pichani) wakati Mawaziri wa Fedha na makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi
wanachama wa Taasisi hizo kutoka Bara la Afrika, walipokutana kama kamati,
Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Dotto James, wakifuatilia kwa makini mkutano wa Magavana wa Benki
ya Dunia kutoka Barani Afrika uliohudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim
Yong Kim, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwa na Waziri wa Fedha wa Swaziland Bw.
Martin Dlamini wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu
(Magavana) kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika, mkutano uliomshirikisha pia
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani, Christine Lagarde (hayupo
pichani), Jijini Washington DC, Marekani.
Wataalamu wa
Fedha na Uchumi Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kutoka Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) wakisikiliza kwa makini mkutano wa Shirika la Fedha Duniani-IMF,
ukisimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Christine Lagarde
(Hayupo Pichani) ambaye aliwambukusha
wajumbe wanaoziwakilisha nchi zao kuwa umasikini bado ni changamoto kubwa na unasababisha vikwanzo vingi katika kukuza
maendeleo na ustawi wa nchi wanachama, Jijini Washington DC-Marekani.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakibadilishana mawazo kabla ya
kukutana na uongozi wa Juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika,
Jijini Washington DC nchini Marekani.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akifafanua jambo alipokutana na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya
Afrika, Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe Hayupo pichani), Jijini Washington
DC-Marekani. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno
Ndulu akifuatiwa na Naibu Gavana wa Benki hiyo Dkt. Natu Mwamba.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (aliyenyoosha mkono)
akielezea jambo wakati Ujumbe wa Tanzania Ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango, kulia kwake, walipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Africa Group I Bw.
Abebe Aemro Selassie (Hayupo pichani) ambapo Gavana alieleza kuhusu uchumi wa sasa wa Tanzania
pamoja na Hali ya uchumi unavyokua kwa kiasi cha kuridhisha, Jijini Washington
Marekani.
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato,
akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kitabu Chenye
maelezo mbalimbali ya miradi inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili wa
shirika hilo, ambapo Japani imeahidi kuendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha
kuendeleza miundombinu ya barabara na sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akiwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James (kushoto) wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la
Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, wakati Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri
wa Fedha na Mipango ulipokutana na Mkurugenzi huyo ambaye ameahidi kuwa Japan
itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii,
Jijini Washington DC, Marekani.
........................................................................................................
........................................................................................................
Benny Mwaipaja,
MoFP
Washington DC,
Marekani
MAWAZIRI wa Fedha
na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi mbalimbali za kiafrika, wanachama wa Benki
ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, wamekutana Jijini Washington DC,
Marekan,i na kuzitaka Taasisi hizo kuweka mipango inayoakisi na kutatua
changamoto zinazolikabili bara hilo ikiwemo, uhalifu, umasikini, mizozo ya
kivita na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi
Aidha, Viongozi
hao wamezitaka taasisi hizo kuweka uwiano wa uwakilishi wa uongozi wa juu ili
kuhakikisha kuwa maslahi mapana ya nchi hizo yanalindwa na maendeleo endelevu yanafikiwa kwa haraka.
Akizungumza kwenye
moja ya mikutano hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambaye
kiutaratibu ni mmoja wa Magavana wa Benki ya Dunia na IMF, amesema kuwa
mashirika hayo ya fedha ya kimataifa yanamchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi za kiafrika ikiwemo
Tanzania.
Hata hivyo amesema
kuwa mdororo wa uchumi duniani, ambao unaonesha kuwa viwango vya ukuaji wa
uchumi vilivyokadiriwa kufikiwa kwa asilimia 3, havitafikiwa ambapo takwimu
zinaonesha kuwa ukuaji wake hivi sasa ni asilimia 1.5 tu, unaashiria namna nchi
wanachama zinatakiwa kujipanga kuhakikisha kuwa uchumi unapanda.
Dkt. Mpango
amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kwa wastani wa asilimia 7 kwa
mwaka lakini changamoto kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa uchumi huo unaonekana
katika maisha ya kawaida ya wananchi wake
“Kila mara
utasikia malalamiko ya wananchi kwamba uchumi wetu unakua kwa namba tu hawaoni
ni kwa kiasi gani uchumi huo wanauona katika maisha yao ya kawaida kwa hiyo ili
uchumi uhesabike kuwa unakua ni lazima uwe jumuishi na ushirikishe watu wengi”
alisema Dkt. Mpango
Amesema kuwa hali
hiyo itawezekana ikiwa sekta zinazochangia maendeleo kwa kasi zaidi kama
kilimo, uvuvi, biashara ya miamala ya simu, miundombinu na viwanda,
zitaimarishwa ili kukuza ajira na kuongeza kipato cha wananchi.
“Tunataka kilimo
kiwe cha kisasa na cha kibiashara kwa kutumia zana na pembejeo bora za kilimo,
uongezaji wa thamani ya mazao na kuwa na masoko ya uhakika ili kukuza ajira
nyingi hususani kwa vijana” Aliongeza Dkt. Mpango
Amebainisha kuwa
Tanzania itaendeleza uhusiano mzuri uliopo kati yake na Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha Duniani-IMF na kuwataka watanzania waelewe kuwa mikopo na
ruzuku zinazotafutwa na serikali yao ni kwaajili ya kuwaletea maendeleo kwa
kuwekeza kwenye miradi yenye tija.