Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa mkoa mara baada ya kuwasili
mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea vituo vya kulea
wazee na watu wasiojiweza vya Chazi na Fungafunga vyote vilivyopo Mkoani huko.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni Ikulu Ndogo Mkoani Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya watoto alipofika kutembelea
makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo
Manispaa ya Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni alipofika katika makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya
Morogoro.
Baadhi ya Viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na
watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro
wakimuonesha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli
maeneo ya miradi yaliyokatika makazi hayo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee wanaoishi katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Regina Chonjo
akiongea na wazee makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya
Fungafunga na kuwataka viongozi wa kituo
hicho kuwasiliana mara kwa mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada
ili kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na
watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akishukuru Mama Janeth
Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa
wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akiongea na Wazee katika makazi ya Kulea Wazee na watu
wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro ambapo
amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu
binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika
kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata
huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na
watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akimkabidhi Mke wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli hotuba.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma ya asili na baadhi ya viongozi wa makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Mke wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi ya Chakula Mwenyekiti wa Wazee wa
makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph
Kaniki.
Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na
watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki. Akimshukuru Mama
Janeth Magufuli kwa msaada wa chakula na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo
kwani kusaidia wazee ni kulisaidia taifa pia.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi
ya kuku kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa makazi ya wazee ya Fungafunga.
18-Baadhi
ya Nyumba Wanazoishi wazee katika Makazi ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya
Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akibadilishana mawazo na mmoja ya wazee katika makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania
Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwaaga baadhi
ya Wazee na watu wenye mahitaji maalum katika makazi ya Kulea Wazee na watu
wenye mahitaji maalum ya Fungafunga.
PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
......................................................................................
NA
HASSAN SILAYO-MAELEZO
Wizara,
Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau
mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu
wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri
iwekenavyo.
Hayo
yamesemwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu
wenye ulemavu alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha
Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.
“Kundi
hili ni moja kati ya makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi
kikubwa ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa
mahitaji muhimu wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za
Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa
maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili
kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama Janeth.
Pia
Mama Janeth alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.
John Pombe Magufuli inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika
kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote
muhimu.
Aidha,
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari
Kilo 175, Maharage Kilo 350 na Mafuta ya
watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama Janeth aliwataka viongozi wa kituo
hicho kuhakikisha chakula hicho kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa.
Akiongea
wakati akimkaribisha Mama Janeth Magufuli, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi.
Regina Chonjo aliwataka ameataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa
mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa
changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.
Naye
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo hicho Bw.Rashid Omar alimshukuru Mama Janeth
Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa
wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.





























0 Comments