Random Posts

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, AHAMAD MASAUNI AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA KUTOA HUDUMA YA MAGARI MAKUBWA NA MADOGO JIJINI DAR ES SALAAM


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Hamad Masauni, akikata utepe kuashira ufunguzi wa kituo kipya cha kisasa cha huduma ya magari madogo na makubwa kilichopo Magomeni Mwembe chai jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, Kushoto ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani ,Mohamed Mpinga na Meneja usambazaji kanda ya Afrika Mashariki Dkt.Fulgence Bube.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Katibu wa baraza hilo ambae pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya maatairi ya Superdoll, Seif Seif (kulia) wakifurahia mara baada ya uzinduzi huo wa kituo cha kisasa kinachotoa huduma za magari. 
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipuliza kifaa maalumu kilichopo ndani ya gari  ambacho ikiwa dereva ametumia kilevi gari hiyo haiwezi kuwaka.


Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), Katibu wa baraza hilo ambae pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya matairi ya Superdoll, Seif Seif(wapili kushoto), wakimsikiliza Msimamizi wa Kituo   baada ya uzinduzi wa kituo kinachotoa huduma za magari upande wa matairi, Paul Kusoga wakati akitoa maelezo ya jinsi ya kulichunguza tairi kutumia mfumo wa komputa.
 Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akimsikiliza kwa makini,Naibu waziri wa mambo ya Ndani ,Mhandisi Hamad Masauni katika hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha kutoa huduma kwa magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni Mwembe Chai jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo kipya cha huduma kwa wateja.
     Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani ,Mohamed Mpinga, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo kipya cha huduma kwa wateja.
        Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mhandis Hamad Masauni, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo cha wateja.
   Mwakilishi wa Michelin kutoka nchini Ufaransa Bw, Samuel Boafo akitoa maelezo juu ya ubora wa tairi ya Bf Goodrich.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kisasa 
Wagani waalikwa wakishuhudia uzinduzi huo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mhandis Hamad Masauni, pamoja na viongozi wengine wakifurahiya burudani ya kikundi cha mziki wakati wa hafla hiyo. 

 Wasanii wa bongo flava wakitoa burudani.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Superdoll wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni mwembe chai jijini Dar es Salaam.



Wafanyakazi wa Kampuni ya Superdoll wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa uzindi wa kituo cha kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni mwembe chai jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Alex John-Mtazamo Media Blog.