
Washiriki
wa mashindano ya KMKM kilomita kumi wanawake na wanaume, wakisubiri
kuanzishwa kwa mbio hizo katika mashindano yaliyoanzia Makao Makuu ya
kikosi hicho Kibweni na kumalizikia Maisara mjini Zanzibar.

Wakimbiaji katika mashindano ya kilomita kumi yaliyoandaliwa na kikosi chaKMKM wakichuana vikali kuelekea mfundani.

Mkimbiaji
Nelson Priver wa timu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Arusha
akifuatiwa na John Leonard pia wa timu hiyo wakiongoza mashindano hayo.

Mkimbiaji
Sarah Ramadhan kutoka Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM),
akimaliza mashindano hayo kwa kushika nafasi ya kwanza kwa upande wa
wanawake katika viwanja vya Maisara.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo ya riadha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa, Serekali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji
Omar Kheri (wa 5 kutoka kulia) akijumuika na viongozi wengine
kuwashangiria wanariadha waliokuwa wakipita mbele yao.

Mjumbe
wa kamati ya maandalizi ya KMKM kilomita kumi CPO. Abdallah Shaaban
akisoma risala ya mashindano kwa mgeni rasmi na wageni walikwa
waliohudhuri katika mashindano hayo.

Mkimbiaji
mkongwa aliyoipa sifa Tanzania Kanali Mstaafu. Juma Ikangaa akitaa
nasaha zake kwa wakimbiaji wa mbio za KMKM kilomita kumi mara tu baada
ya kumalizika kwa mashindano hayo.

Mkuu
wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) Komodoo. Hassan Mussa akitoa
shukrani kwa washiriki wote wa mashindano yaliyoandaliwa na kikosi
chake na kumkaribisha mgeni rasmin.

Mgeni
rasmi katika mashindano hayo ya riadha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa, Serekali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar
Kheri akiwahutubiwa wanamichezo waliomaliza mashindano ya KMKM kilomita
kumi katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar

Mgeni
rasmi katika mashindano ya KMKM kilomita kumi Waziri. Haji Omar Kheri
akimpa zawadi ya pesa taslim laki tano mshindi wa kwanza kwa upande wa
wanawake Sarah Ramadhan.


Mgeni
rasmi katika mashindano ya (KMKM) kilomita kumi Waziri. Haji Omar Kheri
(katikati) waliosimama chini, (kulia) Waziri wa Habari, Utalii,
Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma na (kushoto) Mkuu wa Kikosi cha
KMKM Komodoo. Hassan Mussa wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa
1,2 na 3 wa mashindano ya KMKM kilomita kumi.
Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
0 Comments