Mpiga Golf Sara Denis Amina wa Klabu ya Golf ya Lugalo
Jijini Dar Es Salaam akiwa katika Mazoezi
kujiwinda na Mashindano ya Arusha Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi
karibuni Jijini Arusha Nyuma ni Amina Hamisi,Sophia Mathias wachezaji wenziei
wa klabu hiyo (Picha Na Luteni Selemani Semunyu).
Kapten
wa Klabu ya Golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai (katikati) akitoa maelezo kwa
Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu(OTO) Brigedia Jenerali
Jairos Mwaseba wakati mbelea viwanja vya golf vya Lugalo Jijini Da r es Salaam
katika mashindano ya CDF Trophy 2016.
Mnaadhimu
Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo
(kushoto) Akisalimiana na Meneja wa Klabu ya Golf Lugalo Kanali Gerlard Omary,
mara alipowasili katika Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam kusuhudia
mashindano ya Mkuu wa majeshi
yaliyomalizika hivi karibuni Katikati ni Mwenyekiti wa klabu hiyo Brigedia
Jenerali Michaele Luwongo
Mnaadhimu
Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo
(kushoto) Akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali
Michaele Luwongo mara alipowasili katika klabu hiyo Jijini Dar es Salaam
kushuhudia CDF Ttophy iliyomalizika hivi karibuni.
Baadhi ya Wachezaji Wanawake wa Klabu ya Golf ya Lugalo ya
Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mazoezi kujiwinda na Mashindano ya Arusha
Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha.
( Picha na Luteni Selemani
Semunyu)
............................................................................................
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange ambaye
ni Mlezi wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Golf Club ameimarisha safu ya uongozi wa klabu hiyo kwa
kuwateua Naibu katibu Mkuu na Mkuu wa Miundombinu kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
BRIGEDIA Jenerali Mwamunyange amemteua Kanali Rajabu Mohamed
Mwenyumbu kuwa Naibu Katibu wa klabu na Kapteni Kitego Kuwa Mkuu wa
Miundombinu ya Klabu(Ground Member) kuchukua nafasi ya Kanali Jackson Nsigaye
aliyehamia Bukoba kikazi.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa Klabu
hiyo Generali Michael Luwongo alisema
Hatua hiyo inalenga kuboresha klabu hiyo ambayo inamikakati mikubwa ya
kuboreshwa na kuwa kitovu cha Michezo cha kisasa che nye hadhi ya Kimataifa.
Wakati huo huo wachezji wa Timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya
Lugalo ya Jijini Dar es Salaam wako
katika maandalizi ya mwisho kujiwinda na Mashindano ya Arusha open yanayotarajiwa kufanyika Hivi
karibuni Jijini Arusha.
Akiongea na Waandishi wa Habari katika Klabu hiyo Kapteni
Japhet Masai alisema mashindano hayo
ambayo ni muhimu katika kupandisha viwango vya wachezaji yanatarajiwa kufanyika
Jumamosi na Jumapili ya Oktoba 15 na 16
huku ikihusisha wachezaji wasio wa kulipwa (Amature).
Alisema Klabu ya Lugalo inatarajia kuingiza wachezaji wa Daraja la A,B,C senior huku
wachezaji watoto ambao ni Junior watashindwa kushiriki kutokana na kuwa
mashuleni katika kipindi hichi.
“ Mashindano haya ni Muhimu kwa Wachezaji wetu lakini pia
itatupa fursa kwa wachezaji wetu wenye viwango kupata nafasi kuchezea timu ya
Taifa iwapo wataonekana. Alisema Kapteni Masai.
Kapteni Masai alisema kumbukumbu ya Matokeo mazuri katika
mashindano ya Tanzania open kwa kuchukua
ushindi wa Kwanza na wa Pili gross huku Daraja B ikichukua Ushindi wa Kwanza na
katika mashindano ya Moshi Open kuchukua nafasi ya Kwanza Mshindi wa Jumla.
Kwa upande wake Afisa
Utawala wa Klabu hiyo Kapteni Amanzi Mandengule alisema Jumla ya wachezaji 10
wanatarajiwa kwenda kushiriki michuano hiyo wakiwemo wanawake watatu na wanaume
Saba.
Aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji hao Kitaongozwa na Kapteni Amanzi Mangengule, Kapteni Japhet Masai,
Kapteni Kibuna Shabani, Juma Likuli,Noel Mheni,Nicolous Chitanda ,Michael Obare,
Amina Hamisi,Sara Denis na Sophia
Mathias.
Afisa huyo wa Utawala alisema maandalizi yote yamekamilika
na kinachosubiriwa ni Baraka za Mwenyeki wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali
Michael Luwongo ili kuhakikisha wanakwenda kuwakilisha vyema Jeshi kwa kurejea na Ushindi.




