Ni vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”
NI vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”. Ndiyo unavyoweza kusema kuelekea mpambano wa
waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi.
Onyesho hilo linasosubiriwa kwa hamu kubwa litafanyika
Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar
es Saalam.
Bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na
Mashauzi Classic ndiyo zitakazosindikiza mpambano wa mahasimu hao wawili.
“Sura Surambi” ni moja ya nyimbo ambazo piga ua lazima iwe
kweye ratiba ya Isha Mashauzi wakati iwe isiwe Leyla naye lazima aidumbukize
ngoma yake ya “Nina Moyo Sio Jiwe” katika orodha ya nyimbo atakazotumbuiza.
Tangu onyesho hilo litangazwe, waimbaji hao wameingia kwenye
vita vikubwa vya maneno ambapo kila mmoja amejinasibu kuibuka na ushindi.

0 Comments