Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
............................................
Timu
ya Simba sc tayari imeshatua mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao
dhidi ya Mwadui FC unaotarajiwa kuchezwa mwisho mwa wiki hii huku Kocha
Mkuu Joseph Omog ametamba kuwa wamekuja kuchukua alama tatu muhimu.
Akizungumza
baada ya kutua Shinyanga Omog,amesema kuwa nia yetu ni kuendelea kupata
matokeo mazuri kwa kila mechi tunayokutana nayo na sio kwamba
tunadharau wapinzani ila msimu huu tumejiandaa kutwaa ubingwa mapema na
hiyo ndio kiu ya wanasimba.
"Tumekuja kupamba na kuondoka na
alama zote kwa sababu tuna mechi mbili dhidi ya Mwadui FC na Stand
United hivyo hatukuja kula kutalii na tunajua michezo yote itakuwa
migumu kwetu ila wachezaji wangu wapo kwa ajili ya kupata
ushindi"alisema Omog
Kwa sasa Simba ndio timu pekee ambayo
imecheza mechi kumi na moja bila kupoteza hata mchezo mmoja na
kujikusanyia alama 29 na kuwa kinara wa Ligi huku wachezaji wakiwa na
morali na kiu ya kuchukua ubingwa msimu huu na wanaonekana kuwa na uchu
wa mafanikio.
Ukiangalia kila idara msimu huu imekamilika na
mchezaji yoyote anayeingia anaenda kufanya kazi yake ipasavyo na
kumekuwa na wafugaji wengi pindi wanapopata nafasi ya kutupia na sasa
kinara ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin naye ameibuka ghafla na kila
mechi anacheka na nyavu tu.
0 Comments