Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla
ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana
Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka
kushoto, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za
Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri
wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza
Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840
na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa
mwaka huu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya
kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo
na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara mara
baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi
kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba
katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi
wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake
Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi
Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi wakati brass bendi ya JKT ilipokuwa
ikitumbuiza mara baada ya kukamilika kwa tukio la kuweka jiwe la msingi katika
mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono
wakati akiwasili katika viwanja vya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Taaswira
ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia
asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
PICHA NA IKULU











0 Comments