Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wafanyakazi Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kufungua rasmi kiwanda
cha Usindikaji wa Matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege mkoani Pwani leo Oktoba 6, 2016
PICHA NA IKULU
..................................................................................................................................
Na: Frank Shija, MAELEZO
TENESCO yapewa miezi miwili kuhakikisha inafikisha huduma ya umeme katika ki
wanda cha kusindika
matunda na kuzalisha juisi na vinywaji baridi cha Bakhresa Food Products Ltd
kilichopo Mwandege wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.
Agizo hilo limetolewa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati
wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda hicho iliyofanyika leo wilayani Mkuranga,
Mkoani Pwani.
Amesema kuwa ni ajabu
kwa mwekezaji kuanza ujenzi hadi,anamaliza na baadaye anaanza uzalishaji halafu
suala la nishati ya umeme linakuwa kikwazo hali inayomlazimu mwekezaji kutumia
nishati mbadala (Jenereta) kitu kinachosababisha gharama za uendeshaji kuwa
kubwa.
“Ninaagiza
hakikisheni mnafikisha umeme katika kiwanda hiki kabla ya mwezi wa 12, nia
ajabu sana mtu anaanza kujenga mnamuangalia tu, anamaliza mnamuangalia, Meneja
wa TANESCO upo? Hakikisha umeme unafika kama kuna mtu ana kukwamisha niambie”.
Alisema Rais Magufuli.
Aliongeza ni imani
yake kuwa baada ya umeme kufikishwa katika kiwaanda hicho gharama za undeshaji
zitapungua na kupelekea kufanya maboresho ya maslahi ya wafanyakazi wake.
Katika hatua nyingine
Rais Magufuli ametumia wasaa huo kumuomba Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa
kuangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji kama huo katika maeneo mengine ya
kikanda hili kutoa fursa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kupata soko
la bidhaa zao.
Kwa upande wake Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa uwekezaji
uliofanywa na Makampuni ya Bakhresa unasaidia kuchochea kilimo cha matunda na kutoa
fursa ya soko la uhakika kwa wakulima.
Mwijage alisema kuwa
Sekta ya Viwanda nchini imeendelea kukuwa, aliongeza kuwa adhima ya kufikia
Tanzania yenye uchumi wa kati kutokana na viwanda itatimia endapo
wafanyabiashara wenye viwanda watakua
wazalendo kama Bakhresa.
Naye Mwakilishi wa Kampuni
ya Bakhresa Food Production Ltd Bw. Yusuph Bakhresa ameishukuru Serikali kwa
kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara wenye viwanda nchini, hali ambayo
itasaidia kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya kuitaka Tanzania kuwa
nchi yenye viwanda ifikapo mwaka 2025.


0 Comments