Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na
Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Separatus Fella (wapili kulia-meza kuu), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya
Siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na
biashara ya kusafirisha binadamu. Fella alisema wadau wa warsha hiyo watatoa
elimu kwa umma jinsi ya kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika.
Wapili kushoto meza kuu ni Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa
Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer. Kushoto ni
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi, na kulia
ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Tamara Keating. Warsha
hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa
Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer akitoa
hotuba yake katika Warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na
kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu nchini.
Katikati ni Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na
Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus
Fella, na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Tamara
Keating. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es
Salaam.
Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na
Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Separatus Fella (katikati), akiteta jambo na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya
(EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de
Geer, mara baada ya Katibu huyo kufungua Warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi
ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha
binadamu nchini. Fella alisema baada ya warsha hiyo, washiriki hao wataanza kutoa
elimu kwa umma jinsi ya kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika. Kushoto
ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi. Warsha
hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili
kulia-waliokaa), Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na
Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer (wapili kushoto-waliokaa),
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi
(kushoto-waliokaa), Meneja wa Mradi Umoja wa Ulaya (EU), Anna Costantini,
wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka Taasisi za Serikali pamoja na
Mashirika yasiyokuwa ya Serikali, mara baada ya kufunguliwa warsha ya siku
mbili ya kujadili namna ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na
biashara ya kusafirisha binadamu nchini. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli
ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
......................................................................................................
Na Felix Mwagara, MOHA
SERIKALI kwa
kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa wameanza kujadili nyenzo mbalimbali
ambazo zitasaidia kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya
kusafirisha binadamu nchini.
Akizungumza wakati
akifungua warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia
watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu, inayofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa
Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella alisema warsha hiyo ni
muhimu ikiwa na lengo la kusaidia idadi kubwa ya watoto walioathirika nchini.
Alisema Tanzania ambayo
ni kati ya mataifa yanayoshamiri kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto kwa
lengo la kwenda kuwatumikisha kazi katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na
duniani kwa ujumla, kupitia nyenzo hizo zitakazo jadiliwa zitasaidia kutoa elimu kwa umma juu ya matatizo hayo
nchini.
“Nyenzo hizi za
kuwasaidia na kuwalinda wale watoto walioathirika baada ya kutoka katika maeneo
mbalimbali zitasaidia kutoa elimu ya kuwandaa kisaikolojia ili wasikate tamaa
na maisha, pia watoto watalindwa na baadaye watarudishwa kwa wazazi wao ili
waweze kuendelea majukumu mengine ya kujenga taifa,” alisema Fella na kuongeza;
“Kumekuwepo na wimbi kubwa
la kuwasafirisha wasichana wa Kitanzania kwenda nchi za uarabuni kwa lengo la
kwenda kufanya kazi za ndani, ila wanapofika huko mambo yanawaharibikia wanaanza kudhalilishwa, kunyanyaswa kiasi
kwamba wanashindwa kupata misaada, kutokana na manyanyaso hayo urudi nchini
wakiwa wameathirika kwa kiasi kikubwa.
”
Fella alisema wadau wa
warsha hiyo watatoa elimu kwa umma kuhusu kukomeshwa kwa biashara hiyo haramu
na wazazi kutokuwaruhusu watoto wao kwenda kufanyiwa unyanyasaji huo kwa kuwa
ni kinyume cha sheria. Hata hivyo, kutokana na wimbi hilo kuzidi kushika kasi
nchini, pia wadau hao watatoa elimu ya watoto walioathirika mara baada ya
kurudi nchini ili wajitambue kutokana na mateso mbalimbali waliokumbana nayo
ili wasiweze kukata tama kutokana na vitendo vya ukatili walivyofanyiwa katika
maeneo wanayotoka.
Aidha, Mwakilishi Mkuu
wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla,
Balozi Roeland Van de Geer alisema Tanzania ni kati ya nchi zilizoathirika na
biashara haramu ya kusafirisha watoto, hivyo elimu inahitajika ili kukomesha
biashara hii hatari.
“Watoto wa leo ni
mabibi na mabwana wa kesho, hivyo wapaswa kulindwa pamoja na kuelimishwa, Umoja
wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwasaidia watoto waweze
kuepuka mateso wanayoyapata,” alisema Roeland.
Warsha hiyo iliandaliwa
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na inatarajiwa kumalizika Oktoba 20
mwezi huu ambapo wadau hao wataanza kufanyia kazi nyenzo hizo zilizojadiliwa.




0 Comments