Katibu Muhtasi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Fatma Saadat akimvisha
Koja la Mauwa aliekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo Bi. Mwanahija
Almasi Ali katika sherehe ya kumuaga iliyofanyika eneo tengefu Saateni Mjini
Zanzibar. Bi Mwanahija kwa sasa ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.
Wanafunzi wa Madrasa wakisoma Dua maalum ya kumuaga aliekuwa Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Shirika la Biasha la Taifa Zanzibar (ZSTC)Bi. Mwanahija Almasi
Ali iliyofanyika eneo tengefu Saateni Mjini Zanzibar.
Wafanyakazi wa Shirika la Biashara la
Taifa Zanzibar (ZSTC) na wageni walikwa wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji
wa Shirika hilo Dkt. Said Seif Mzee (alievaa shati jekundu) wakiitikia Duwa
maalum ya kumuaga aliekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZSTC Kassim Maalim Suleiman akimkabidhi
Cheti cha utendaji kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la (ZSTC) Bi.
Mwanahija Almasi Ali katika sherehe iliyofanyika eneo tengefu Saateni Mjini
Zanzibar. (Katikati) Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo Dkt. Said Seif Mzee.
Mgeni rasmi aliekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biasha la Taifa
Zanzibar (ZSTC)Bi. Mwanahija Almasi Ali akizungumza na wafanyakazi na wageni waalikwa
katika sherehe aliyoandaliwa na wafanyakazi wa Shirika hilo.
Mgeni rasmi (katikati) waliokaa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
wa wa Shirika hilo.
Picha na
Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.





