Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
Profesa Justin Ntalikwa.
..................................................................................................................
Na
Greyson Mwase, Mtwara
Ili
kuondokana na adha ya kuharibiwa kwa miundombinu ya umeme ikiwa ni pamoja na
nguzo kuchomwa na moto pindi wananchi
wanaposafisha mashamba, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limetakiwa kuanza
matumizi ya nguzo za zege badala ya nguzo za miti.
Hayo
yalielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin
Ntalikwa alipokuwa akizungumza na uongozi wa
TANESCO mkoa wa Mtwara alipokuwa katika ziara ya siku tatu katika mkoa
huo kwa ajili ya kukagua shughuli za nishati
husuan maeneo gesi inapozalishwa
pamoja na madini.
Alisema
kumekuwepo na changamoto ya nguzo za
umeme kuchomwa moto hususan katika kipindi cha kiangazi wananchi
wanaposafisha mashamba yao, sehemu
nyingi nchini husuan katika maeneo ya
vijijini.
Alisisitiza
kuwa pamoja na elimu kutolewa kwa wananchi
juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme hususan nguzo, bado kuna haja ya
TANESCO kuwa wabunifu kwa kuanza kutumia nguzo za zege ambazo haziungui kwa haraka na kuepusha hasara ya kuchomwa na
moto
“
Fedha inayotumika kwa ajili ya kurudisha nguzo zilizochomwa na moto ingeweza
kupeleka umeme katika maeneo mengine
ambayo hayana huduma ya umeme,”alisema
Profesa Ntalikwa.
Aidha,
aliwataka watumishi wanaofanya kazi katika ofisi za TANESCO kuacha mazoea ya
kukaa ofisini na kusubiri wateja na badala yake wanatakiwa kuwafuata wateja
majumbani na kuwashawishi kuunganishwa na huduma za umeme.
“
Ni lazima mhakikishe shirika la TANESCO
linaongeza mapato yake na kujiendesha kwa faida na sio kwa hasara, muwafuate
wateja majumbani badala ya kukaa ofisini tu,” alisisitiza Profesa Ntalikwa.
Pia,
Profesa Ntalikwa aliwataka watumishi wa
TANESCO kuhakikisha kuwa wateja wanaoomba na kulipia huduma za kuunganishiwa umeme wanaunganishiwa ndani ya
mwezi mmoja badala ya kukaa kwa muda mrefu
hali inayokatisha tamaa.
Alisema
kuwa mteja ana haki ya kuunganishiwa huduma ya umeme kwa wakati pindi anapokamilisha taratibu zote
za malipo.
Awali
akizungumzia hali ya umeme na utekelezaji wa miradi ya umeme katika mkoa wa Mtwara kupitia taarifa yake, Meneja wa Shirika la Umeme Mkoa wa Mtwara,
Mhandisi Azizi Salum alisema kuwa umeme unaotumika katika mikoa ya Lindi na
Mtwara unazalishwa kutoka katika mitambo
ya TANESCO iliyopo Mtwara Mjini inayotumia gesi ambapo kwa sasa
inazalisha Megawati 18 huku matumizi ya
juu yakiwa ni Megawati 15.1
Alisema
kuwa, hadi kufikia mwezi Septemba, mwaka huu
mkoa ulikuwa na jumla ya wateja 30,457 ambapo wateja wakubwa
katika mkoa wa Mtwara wakiwa ni 44.
Akielezea
jitihada zilizofanywa na shirika la TANESCO katika upunguzaji wa matukio ya kukatika kwa umeme katika wilaya za Lindi na Mtwara, Mhandisi Salum alieleza
kuwa ni pamoja na ubadilishaji wa nguzo
chakavu na vikombe vilivyopasuka katika maeneo ya Newala kuelekea Masasi
hadi Ndanda ambapo kati ya Julai na
Septemba mwaka huu jumla ya nguzo 300
zilibadilishwa.
Aliendelea
kusema kuwa kazi nyingine zilizofanywa ni pamoja na ufungaji wa vikata umeme
kwenye vipande vya njia za umeme vilivyo virefu na ujenzi wa njia ya
kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti
132 yenye urefu wa kilometa 80 na ufungaji wa transfoma ya ukubwa wa 20MVA
132/33kV eneo la Migoyo ili kuboresha upatikanaji wa umeme katika manispaa ya
Lindi na wilaya za Masasi, Nachingwea na
Ruangwa.
Aidha,
akielezea miradi mingine ya umeme
iliyotekelezwa katika mkoa wa
Mtwara, Mhandisi Salum alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja ujenzi wa
miundombinu ya umeme vijijini
chini ya ufadhili wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao
ulihusisha ujenzi wa njia ya umeme
Msongo wa kilovolti 33 wenye jumla ya kilometa 213 na ufungaji wa transfoma 38
ambapo gharama ya mradi ilikuwa ni shilingi bilioni 9.477 na kuongeza kuwa
ulikamilika mwezi Juni mwaka huu
Miradi
mingine ni pamoja na mradi wa kupeleka umeme kwenye wilaya za Tandahimba,
Mtwara Vijijini na maeneo yaliyo katika
mkuza wa bomba la gesi chini ya mkandarasi Namis Corporate LTD
Alisema
mradi huu wenye gharama ya shilingi
bilioni 19 unahusisha ujenzi wa kilometa 304.92 za msongo wa kilovolti 33, ufungaji
wa transfoma 106, ujenzi wa njia za
kusambazia umeme jumla ya kilometa 265.15 na kuunganisha wateja 9,037
katika vijiji na vitongoji 83
Alisisitiza
kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha
2016/17 shirika la TANESCO limetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.078 kwa ajili ya kusambaza huduma
ya umeme katika maeneo mbalimbali ya
mkoa wa Mtwara.

0 Comments