Usiku
wa saa tatu,Oktoba 12.2016 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na
familia kwa ujumla wamepokea kwa masikitiko kuhusu kifo cha Kada wa Muda
mrefu wa Chama hicho, Dkt Didas Masaburi.
Masaburi
amekuwa kada mtiifu ndani ya chama chake alikuwa mtu mahiri kwenye
uchaguzi wa ndani ya chama kuliko hata sekta nyingine ni dhahiri kuwa
alikifia chama.
Amewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam sambamba na kuwa Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki.
Dkt
Masaburi ni miongoni mwa viongozi wa CCM walioivishwa ukada kutokea
Umoja wa Vijana UVCCM enzi hizo akiwa makini kabisa yeye, marehemu
Rashid Mchatta na William Vangimembe Lukuvi.
Kifo chake kimejiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anapatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Taarifa za awali zimebaini kuwa msiba upo nyumbani kwake Segerea Jijini Dar es salaam.

Marehemu Dkt Didas Masaburi.
