Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
................................
Shirikisho
la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kuwa bado hawajapokea
baraua kutoka katika baraza la michezo la taifa BMT kuhusiana na taarifa
yake ya usitishwaji wa mfumo wa mabadiliko yanayotakiwa kufanywa na
vilabu vya Simba na Yanga.
Afsa
Habari wa TFF,Alfred Lucas, amesema kuwa ingawa bado hawajapokea barua
hiyo kwa ajili ya kuziwasilisha kwa vilabu husika lakini kama wao
wasimamizi wa mpira wa miguu wanaendelea kuheshimu maamuzi hayo ya
serikali.
Juma
lililopita katibu mkuu wa BMT Mohamed Kiganja alisema kwamba baraza
hilo limestisha mfumo wa hisa na ukodishwaji kwa vila vya Simba na Yanga
kwa kuwa vilabu hivyo havijafuata taratibu za katiba zao,hivyo
wanatakiwa kusitisha hadi hapo watakapoanza kufuata taratibu za sheria
na katiba zao.
Hatua ya Serikali kusitishwa kwa mchakato huu ni
kuwa kuna malalamiko mengi yanatolewa na baadhi ya wanachama
kutokubaliana na jambo hilo huku wengine wakikimbilia mahakamani kupiga
mchakato mzima unaohusiana na mabadiliko yanayotakiwa na vilabu vya
Simba na Yanga.

0 Comments