Random Posts

TIMU YA GOLF YA LUGALO YATESA MASHINDANO YA PWC TROPHY

 n2
Katibu  Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima aliyeshinda  kwa Senior akipiga mpira wakati wa mashindano ya PWC Trophy yaliyofanyika  Jumamosi Oktoba 22 katika uwanja wa Golf wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo Jijini Dar Es Salaam.
n3
Baadhi ya Watoto  (Junior) wa Klabu ya Golf ya  Lugalo walioshiriki mashindano ya PWC  Jumamosi Oktoba 22 Jijini Dar es Salaam wa Pili Kulia ni Mshindi wa  Kwanza wa Kundi hilo Almadius Simon wa Klabu ya Lugalo.
n4
Wachezaji wa Golf kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima, Dk Edmund  Mndolwa  aliyekuwa Mkuu wa majeshi   Jenerali  Mstaafu George Waitara na Balozi Clemence Sanga wakibadilshana mawazo kabla ya kuanza mashindando ya PWC yaliyofanyika  Jumamosi  Oktoba 22 katika Uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam.
n1
Mshindi wa Jumla wa mashindano ya PWC yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22  Jijini Dar es Salaam  Nicholous Chitanda wa Lugalo aliyeshika Vikombe akiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa  Kushoto ni mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo , wa kwanza kulia ni  Mwenyekiti wa TGU Joseph Tango  na wa pili kulia ni Msuya Mkurugenzi PWC .

(Picha na Luteni Selemani  Semunyu).
.........................................................................................................................
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

 Mchezaji wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  ya Lugalo  Nicholous Chitanda imeibuka washindi wa Jumla katika mashindano ya wazi ya PWC Trophy  yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 katika uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Chitanda aliibuka na ushindi huo nakuwashinda wachezaji wengine zaidi ya 100 waliojitokeza kutoka Klabu zote  Nchini baada ya kupata  Mikwaju au Gross 74 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni Tisa na hivyo kuibuka na Mikwaju ya Jumla Net ya  65.

Katika Division A ushindi ulinyakuliwa na Isack wanyenche kutoka Klabu ya Arusha   baada kupiga mikwaju 69 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni Tatu  na hivyo kuibuka na ushindi kwa kupiga mikwaju ya jumla 66 na kufuatiwa na Juma Likuli wa Lugalo baada ya  kupiga mikwaju ya jumla 68.

Kwa upande wa Division B  mshindi ni Dk  James  Legg wa Lugalo baada ya kupiga mikwaju  84 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 13 na hivyo kuwa na mikwaju ya jumla 71 na kufuatiwa na Salum Mvita wa Dar es Salaam Gymkhana kwa  mikwaju ya Jumla  71.

 Division C kwa upande wake Mpiga Golf Reneir Kuhcmanu wa Lugalo aliibuka na ushindi katika kundi hilo baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 68 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 24 akifuatiwa na Kapten Amanzi Mandengule wa Lugalo pia baada ya kupata mikwaju ya Jumla 69 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 19.

Kwa upande wa Kundi la Wazee ama Senior Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Mh Job Masima alishinda kwa kupiga Mikwaju ya Jumla 75 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 18 akifuatiwa na Balozi Clemence Sanga aliyepiga mikwaju ya Jumla 78 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 16.

Wanawake kwa upande wa kundi lao Chiku Elias wa Lugalo aliibuka na Ushindi kwa Mikwaju ya JUmla 76 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 10 na kufuatiwa na Vicky Elias wa Lugalo kwa  mikwaju ya Jumla 78 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni Nane.

Katika Upande wa  Wachezaji wa Kulipwa Nuhu Mollel wa Arusha aliibuka Mshindi ,watoto  Junior  Almadious Simon wa Lugalo aliibuka na Ushindi baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla  70 na kwa upande wa Wachezaji wasaidizi au Cardes   Hendrick Nyenza wa Lugalo aliibuka Mshindi kwa  Mikwaju 78 akifuatiwa na Deo Hassan wa Lugalo.

Post a Comment

0 Comments