
Mbunge
wa Kasulu vijijini Mhe Augustine Vuma (Kushoto) akitoa maelezo kwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
January Makamba wakati viongozi hao walipotembelea kambi ya wakimbizi
ya Nyarugusu. (Katikati ni Bw. Peter Bulugu Kaimu Mkuu wa Kambi -
Nyarugusu

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba akihutubia katika Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kagera
Nkanda, Wilayani Kasulu

Sehemu
ya wawakilishi wa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi ya
wakimbizi ya Nyarugusu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) mara
baada ya kutembelea kutembelea kambi ya Nyarugusu na kutoa maelezo
katika sekta ya mazingira
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi wakikagua
uharibifu wa mazingira katika msitu wa Makere katika Wilaya ya Kasulu
........................................................................................................
Na Lulu Mussa Kasulu
Imebainika
kuwa ongezeko kubwa la idadi ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu
inachangia kwa kiasi kubwa la uharibifu wa mazingira kwa kuongeza
matumizi ya rasilimali za asili.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu Bw. Peter Bulugu
wakati wa kuwasilisha taarifa ya hali mazingira katika kambi hiyo kwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
Kaimu
Mkuu wa Kambi wa Nyarugusu Bw. Peter Bulugu amesema kuwa hali ya
mazingira katika kambi si nzuri na inakabiliwa na tatizo la uharibufu wa
mazingira kwakuwa wengi wa wakimbizi hao hutumia kuni kama nishati ya
kupikia.
Hata
hivyo Bw. Bulugu amebainisha kuwa Ofisi yake imeeanda mkakati wa
upandaji miti ili kunusuru maeneo yanayozunguka, na kwakuanzia jumla ya
miche 900,000 imeoteshwa katika vitalu. Pia Kambi imedhamiria kugawa
majiko banifu ambayo yatatumia nishati kidogo na uzalishaji wa nishati
kwa kutumia takataka za mashambani unatarajiwa kuanza mwezi Novemba.
Aidha,
mkakati mwingine ni ujenzi wa nyumba za tofali mbichi na kuezeka kwa
mabati badala ya miti ambapo jumla ya nyumba 800 zimekamilika na nyumba
542 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi. Alisema Bw. Bulugu
Akiwa
katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Waziri Makamba ametembelea kambi
ya wakimbizi ya Nyarugusu na kupata fursa ya kuongea na wawakilishi wa
mashirika mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi hiyo.
Waziri
Makamba amesema kuwa ni vema uongozi na mashirika yanayotoa misaada
katika kambi hiyo kuandaa mpango mzuri wa namna ya kuwapokea na
kuwahifadhi wakimbizi ili ujio wao usiathiri watanzania wanaozunguka
kambi ili shughuli zao za uzalishaji mali kila siku ziwe na tija.
Waziri
Makamba aliuagiza Ungozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na
wakimbizi kutafuta pesa zaidi ili mpango wa kugawa majiko banifu
uwafikie wakimbizi wote. "Kaya zilizopo hapa ni 30,000 ninyi mnataka
kugawa majiko hayo kwa kaya 3000 tu, nashauri muangalie uwezekano wa
kugawa kwa kaya zote" Makamba alisisitiza.
Waziri
Makamba pia ameagiza kufanyika kwa Ukaguzi wa Mazingira (Environment
Audit) ndani ya wiki mbili kwakuwa ni takwa la kisheria. Na kuwataka na
kupanda miti kwa wingi. " Pandeni miti ya aina mbalimbali mfao miti ya
matunda, kuni na mbao ili kunusuru mazingira yetu".
Waziri
Makamba pia alitembelea msitu wa Makere wenye takriban ekari 75,000
ambao kwa upande wa Makere kusini kumekuwa na uharibufu mkubwa wa
mazingira na kuagiza doria za mara kwa mara ili kudhibiti wananchi
wanaofanya kilimo cha kuhamahama, kukata na kuchoma miti pia kudhibiti
ongezeko la mifugo kwa kuiandikisha ili mgogoro uliopo baina ya hifadhi
na wananchi uweze kupatiwa ufumbuzi kwa kujenga hoja madhubuti.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na
Mazingira Mhe. January Makamba hii leo ameendelea na ziara ya kukagua
hali ya mazingira katika Mikoa 10 hapa nchini ambapo leo ni siku ya 13.
Waziri Makamba pia atatembelea Mkoa wa Tabora.
0 Comments