
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo
kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo
pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa
mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es
salaam.

Mwakilishi
wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi akielezea mikakati ya KAIZEN kwa
wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo
pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa
mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es
salaam.

Baadhi
ya wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi
wakipokea tuzo zao wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN
Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo
jijini Dar es salaam.

Mgeni
rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu
toka kushoto waliokaa) pamoja na Balozi wa Japan nchini na Mwakilishi
wa JICA Tanzania wakiwa katia picha ya pamoja na wawakilishi wa
mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi walioshinda tuzo wakati wa
sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya
kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
......................................................................................................
Na. Eliphace Marwa – Maelezo
Watanzania watakiwa kuongeza thamani na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini.
WAZIRI
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka watanzania
kuongeza thamani ya bidhaa na uzalishaji ili kuongeza fursa za ajira.
Mwijage
ameyasema hayo wakati akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya
kiserikali na makampuni binafsi wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili
za KAIZEN zinazoratibiwa na Shirika la uhusiano wa kimataifa laJapan
(JICA).
“Tuko
hapa hii leo kushuhudia sherehe za utoaji wa tuzo katika sekta ya
viwanda ambayo ni matunda ya dhana za KAIZEN kwani tuzo hizi zinatolewa
kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kutekeleza mbinu za KAIZEN ili
kuweza kutoa changamoto kwa makampuni mengine” alisema Mh. Mwijage
Kwa
upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA ofisi ya Tanzania Bw. Toshio Nagase
aliipongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na kitengo
cha KAIZEN Tanzania kwa kuandaa sherehe yenye mafanikio kwa mara
nyingine kufuatia ili iliyofanyika mwaka jana.
“Baada
ya uzinduzi wa mpango wa miaka mitano, sisi sote tumetambua umuhimu wa
kukuza viwanda ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa
Tanzania”, alisema Bw. Toshio
Aidha
Bw. Toshio alibainisha baadhi ya maeneo ambayo KAIZEN imefanikiwa kuwa
ni pamoja na kuhakikisha ubora wa bidhaa na kubadilisha tabia pamoja na
kutoa motisha kwa wafanyakazi.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi amesema
kuwa anaamini kuitangaza KAIZEN nchini Tanzania ni jambo la muhimu ili
kutengeneza viwanda vyenye ushindani na kufanikisha lengo la kukuza
viwanda kuelekea mwaka 2025.
0 Comments