Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba akipata maelezo kutoka kwa Bw.
Leonard Kushoka wa pili kulia katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa nishati
mbadala
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiangalia
mkaa uliokamilika baada ya uzalishaji, mkaa ambao ni rafiki kwa
mazingira.
.............................................................................................
Na Lulu Mussa
TABORA
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Jauary
Makamba amempongeza Bw. Leordard Kushoka kwa kubuni kiwanda kinachotengeza
nishati mbadala rafiki kwa mazingira.
Akiwa Mkoani Tabora,
Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea kiwanda hicho na kusema kuwa
Serikali inathamini sana ubunifu na uvumbuzi hasa unao okoa mazingira.
"Bwana Kushoka mimi nakupongeza sana, niliona jitihada zako kupitia
kipindi cha televisheni na kuamua kukuita na kukusaidia" alisisitiza
Waziri Makamba.
Katika kuthamini
mchango wa Kiwanda hicho cha "Kuja na Kushoka" Ofisi ya Makamu wa
Rais imemsaidia Bw. Kushoka kupata haki miliki ya Kiwanda hicho.
Awali Bw. Leonard
Kushoka, Mkurugenzi wa Kuja na Kushoka Tools Manufacture Group amesema kuwa
kiwanda chake kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 13 na kufanikiwa kubuni
teknolojia mbalimbali rafiki kwa mazingira ambapo mpaka sasa wamefanikiwa
kuwafikia vijana zaidi ya 50 katika Wilaya za Tabora Manispaa, Urambo, Kaliua,
Mlele pia Katavi na kufanikiwa kuwafundisha utengenezaji wa Majiko banifu
yanayopunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa asilimia 50.
Pia Kiwanda hicho kimefanikiwa
kubuni mashine ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha kilo 160 kwa saa kwa
kutumia dizeli lita 5 na kuzalisha wastani wa Kilo 1000 za mkaa mbadala na pia
Kiwanda hicho kimefanikiwa kubuni mtambo kwa kukaushia tumbaku kwa kutumia taka
kavu au mabaki yote ya mazao kama maganda ya karanga, randa za mbao, magunzi ya
mahindi na masuke ya mpunga.
Bw. Kushoka amesema
kuwa "Mtambo huu umetoa matokeo mazuri katika ukaushaji wa tumbaku kwani
wastani wa matumizi ya taka kilo 3 hukausha kilo moja ya tumbaku kwa kutumia
mabani ya kisasa"
Bw. Kushoka
amemuomba Waziri kuisaidia Kampuni hiyo kupata mafunzo mbalimbali ya namna bora
zaidi ya kubuni na kuendeleza uzalishaji wa nishati mbadala hasa katika nchi
zinazofanya vizuri zaidi.
'Kuja na Kushoka"
ilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kupata usajili mwaka 2013 na kupewa hati
(TMC/CO/CBO/48).
Waziri Makamba akiwa
katika Mkoa wa Tabora pia amepata fursa ya kutembelea Wilaya ya Nzega na
Igunga, akihitimisha ziara yake ya Mikoa 10 hapa nchini yenye changamoto za
kimazingira.



0 Comments