Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo
pichani), wakati wa kikao cha kujadili
masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho
kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu,
akizungumza wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na
maendeleo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi na Idara zake. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu
Nchemba (hayupo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
John Minja. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini
Dar es Salaam .
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


