Timu
ya African Lyon imeharibu sherehe za Simba katika uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam baada ya kuwatandika goli 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya
Tanzania bara na kuvunja mwiko wa wekundu wa Msimbazi kucheza bila
kufungwa.
Kwa
matokeo hayo yameifanya Lyon kufunga pazia la mzunguko wa kwanza kwa
ushindi mnono na Simba walikuwa wamecheza mechi 13 bila kupoteza hata
mchezo mmoja msimu huu.
Aliyepeleka
kilio Msimbazi ni kinda la zamani la Yanga B,Abdallah Msuhi dakika za
majeruhi 90 baada ya uzembe wa beki pamoja na kipa wa Simba
kujichanganya na kumkuta mfungaji katika nafasi nzuri na kuipandisha
Lyon nafasi ya tisa wakiwa na pointi zao 17.
Licha
ya kufungwa Simba inabaki kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwa na pointi
35 na mchezo wao wa mwisho wa kufunga mzunguko wa kwanza wanaenda
kumaliza mkoani Mbeya dhidi timu ya Tanzania Prisons mchezo utakaopigwa
uwanja wa Sokoine siku ya Jumatano.
Simba
wanatarajia kusafiri kesho kuelekea mjini Mbeya kucheza na Prisons
ambao nao wamejeruhiwa kwa kufungwa na mabingwa watetezi Yanga goli moja
kwa bila lililofungwa na Simon Msuva na kufanya tofauti ya pointi 5 ya
Ligi hiyo.
0 Comments