Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa
madawati yenye tahamani ya Sh. Milioni 20 yaliyotolewa na shule za Al
Murtazir, ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya Mkuu wa Mkoa huyo kuhakikisha watoto
wote wanakaa kwenye madawati leo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad
Mussa Salum akizungumza machache kwenye hafla ya kukabidhi Madawati yenye jumla ya
thamani ya milioni 20 yaliyotolewa na shule za Al Murtazir, ikiwa ni
kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa huyo
kuhakikisha watoto wote wanakaa kwenye madawati leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul
Makonda akikata utepe kwenye hafla ya kukabidhiwa wadawati leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akikabidhiwa madawati na Mwekiti wa Bodi ya
Elimu ya Shule za Al Murtazir Azim Dewji ili kuunga mkono juhudi za serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ambae pia alikuawa mwalimu Mh.John Pombe Mgufuli
Sehemu ya
wazazi na wanafunzi wa Shule ya Al-Mutanzil leo jijini Dar es Salaam.Picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamiii.
...................................................................................
Idadi ya Wataalamu wa Sayansi imekuwa ikikua
kwa kasi kutokana na sekta hiyo kuwa chanzo cha maendeleo na ugunduzi na kufanya
kupata maendeleo.
Hayo
yamesemwa na Mkuu na Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya
Kukabidhiwa Madawati yenye thamani ya Sh. milioni 20 kutoka kwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Elimu ya Shule za Al Muntazir, Azim Dewj
"Nimeomba
sana wazazi kuhamasisha watoto wao kusoma sayansi, ukifanikiwa kwenye hayo
masomo sio kwamba tu utaajiriwa lakini utaajiriwa sehemu unayoitaka kutokana na
ajira kuwa nyingi ukitofautisha na masomo tuliyosoma sisi,"amesema
Makonda.
Nae Mwenyekiti
wa Bodi ya Elimu ya Shule za Al Muntazir,Azim Dewji amesema ‘’tumeona litakuwa
jambo la busara kama tutaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano tano
inayoongozwa na Rais dk. John Pombe Magufuli ambaye pia alikuwa mwalimu.





0 Comments