Na matukiodaimaBlog
BARAZA kuu la umoja wa
wanawake mkoa wa Iringa limempongeza mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa kuwa
kiongozi wa mfano ndani ya mkoa na nje ya mkoa wa Iringa na hivyo
kumwomba kugombea tena nafasi hiyo ya uenyekiti mwakani 2017 .
Akitoa
pongezi hizo leo wakati akishukuru kwa niaba ya wajumbe wa baraza
kuu la UWT mkoa lililokutana kwenye ukumbi wa CCM wilaya ya Iringa
mjini ,mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini ambae pia
ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) alisema kuwa
ushindi mkubwa ambao CCM iliupata katika uchaguzi mkuu mwaka jana
uchaguzi uliomwezesha Rais Dkt John Magufuli kushinda kwa kishindo
dhidi ya wapinzani wake ni pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na
Msambatavangu katika kampeni za uchaguzi mkuu .
Mkini
alisema mkoa wa Iringa kwenye uchaguzi huo uliweza kufanya vizuri
kwa kushinda majimbo 6 kata ya 7 yaliyopo ndani ya mkoa wa Iringa
na kuwa pamoja na kila mmoja kushiriki katika kupigania ushindi huo
wa chama ila wao kama wanawake hawanabudi kumpongeza mwanamke
mwenzao ambae ndie mwenyekiti wa chama mkoa kwa kuonyesha Taifa kuwa
wanawake wanauwezo wa kuongoza .
''
Naomba kuchukua nafasi hii kwa niaba ya wanawake wenzangu
kukupongeza sana mwenyekiti wetu wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu
umeonyesha mfano mzuri kuwa unaweza kuongoza .......nakumbuka wakati
wa kampeni wewe ulisimama kidete kuhakikisha chama kinashinda
kwa kishindo mbali ya figisu figisu zilizokuwa zikielekezwa kwao ila
hukuteteleka ''
Mbali
ya mwenyekiti kufanya vema katika kampeni za 2015 ila hajaacha
kuitumikia vema jamii ya mkoa wa Iringa ikumbukwe mkoa umepata
misiba miwili mikubwa ukiwemo wa aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM
mkoa Tasili Mgoda na mwasisi wa maendeleo ya wilaya ya Mufindi
Joseph Mungai shughuli zote zimeratibiwa vema na Msambatavangu tena
pasipo ubaguzi wowote .
''
Mwenyekiti wetu anafanya kazi vizuri ndani ya mkoa wetu tena
pasipo ubaguzi wowote na ni mtetezi mzuri sana kwa wanawake ndani
ya mkoa na hanaga unafiki kabisa kwani yeye siku zote husema
kweli tupu ''
Mkini
alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wake mzuri ndani ya
chama wao wanaona bado mwenyekiti huyo anauwezo wa kuwavusha wana
CCM kwa miaka mingine mitano ijayo hivyo kumshawishi kuingia tena
ulingoni mwakani 2017 katika uchaguzi mkuu wa viongozi ngazi mbali
mbali za chama .
Mwenyekiti
wa UWT mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi akisoma tamko la UWT mkoa
wa Iringa kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt Magufuli alisema kuwa
wao kama wanawake wa CCM wameendelea kufurahishwa na utendaji kazi
wa Rais Dkt Magufuli na kuwa kubwa zaidi ni jinsi Rais alivyoweza
kujibu maswali ya watanzania kupitia mkutano wake wahariri wa
vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini.
.Kwa
upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa ,Msambatavangu pamoja
na kupongeza pongezi za baraza hilo dhidi yake na zile za Rais
alisema atahakikisha pongezi za wanawake hao zinamfikia Rais Dkt
Magufuli huku akisisitiza wanawake kuendelea kuongoza nafasi zao
kwa kujiamini zaidi badala ya kutanguliza uoga usio wa lazima .
Alisema
wakati chama kinajiandaa kwa chaguzi zake mwakani ni vizuri
wanawake kuanza kujipima ama kuwapima wale ambao wanaingia kuwania
nafasi mbali mbali ili kupata viongozi wenye uwezo wa kuwatumikia
wananchi hasa katika kipindi hichi cha kujenga chama chenye nguvu
na uongozi wenye uwezo wa kuendana na kauli mbiu ya Rais ya hapa
Kazi tu.
Kwani
alisema wapo baadhi ya watu ndani ya CCM kazi yao ni kusubiri
uchaguzi hadi uchaguzi kufanya kazi za chama na kuwa wanachama hao
hawapo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi bali wapo kwa ajili ya
kutumikia matumbo yao jambo ambalo halikubaliki kwa uhai na nguvu ya
CCM .
Mwenyekiti
huyo alisema hivi sasa wananchi wanauelewa mkubwa juu ya siasa
na uongozi hivyo ni lazima wanaopewa nafasi za kugombea ni lazima
wawe wanakubalika katika jamii inayowazunguka vinginevyo chama
kinaweza kuyumba iwapo watu wasio na sifa watapewa nafasi za
kugombea hivyo ni vizuri kuanza kuwatafuta watu wanaofaa ambao
hawapo ndani ya CCM kujiunga na CCM ili mbeleni waje kugombea
kupitia CCM.
Kwani
alisema hivi sasa kote duniani ni vema viwili pekee ndivyo
vimebaki kuitwa vyama tawala na vyama hivyo ni nchini China na
Tanzania pekee ila maeneo mengine yote vyama tawala imeondolewa
madarakani kwa kuwa CCM lengo lake ni kuendelea kuongoza ni
vizuri kila mwanachama na kila kiongozi kuhakikisha anawajibika vema
kwa wananchi kama ambavyo mwenyekiti wa chama Taifa Rais Dkt Magufuli
anavyoliongoza Taifa kwa faida ya watanzania na vizazi vijavyo.
|
0 Comments