Random Posts

ENGLAND KAA MBALI NA WATOTO YAIFANYIA UNYAMA SCOTLAND,KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018.

Katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu kombe la Dunia nchini Urusi Mwaka 2018,timu ya Uingereza imewachakaza mahasimu wao Scotland kwa idadi ya magoli 3-0.

Daniel Sturridge alikuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabaki wa Uingereza katika dakika ya 23 akifunga goli la utangulizi akipokea mpira toka kwa Kelly Walkers baada ya kuingia kwa goli hilo Scotland walicharuka na kuendelea kulisakama lango la wenyeji hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ili ziweze kuibuka na ushindi mnamo dakika ya 50 kiungo mshambuliaji wa Liverpool Adam Lallana alifunga goli la pili huku akipokea pasi ya Daniel Rose na kuwafanya Scotland kuendelea kuwa wanyonge.

Gary Cahill alipeleka msumari wa mwisho dakika ya 63 kwa kichwa mpira uliopigwa na Nahodha Wayne Rooney na kuweza kuwapa pointi tatu muhimu na kujiweka nafasi nzuri ya kufuzu hadi mpira unamalizika Uingereza wameibuka na ushindi wa magoli 3-0.

Kwa matokeo hayo vijana wa kocha Gareth Southgate wafikishe pointi 10 na kukaa kileleni wakiwa wamecheza mechi nne kushinda tatu na sare moja.

VIKOSI:ENGLAND(4-2-3-1):Hart, Rose, Stones, Cahill, Walker, Dier, Henderson,Lallana, Rooney, Sterling, Sturridge, (Vardy.

Subs not used: Heaton, Clyne, Walcott, Jagielka, Bertrand, Townsend, Kane, Rashford, Wilshere, Lingard, Pickford

Booked: Cahill, Rooney

Goals: Sturridge 24, Lallana 50, Cahill 61

SCOTLAND (4-2-3-1): Gordon, Anya, (Paterson ), Wallace, Hanley, Berra , Morrison (McArthur), Brown, Darren Fletcher , Forrest , Snodgrass  (Ritchie ), Griffiths.

Subs not used: Marshall, Chris Martin, Russell Martin, Naismith, Steven Fletcher, Bannan, Burke, Kingsley, Hamilton

Booked: Griffiths

Referee: Cuneyt Cakir (Turkey) 6.5

Attendance: 87, 258

Player ratings by Sami Mokbel


Post a Comment

0 Comments