Miss Tanzania 2016 Bi. Diana Edward Luqumay.
................................................................................
Na
Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amesema serikali
haijamtelekeza mshindi wa shindano la Urembo la Tanzania kwa mwaka 2016 bali wanaendelea
kumpa msaada wa hali na mali ili kufanikisha ushiriki wake katika mashindano ya
urembo ya dunia.
Mhe.
Nape ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi Bendera ya Taifa
kwa mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano ya Miss Afrika
2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu.
“Haiwezekani
Serikali ikabariki mchakato mzima wa Miss Tanzania mshindi akapatikana alafu akatelekezwa
na tukakaa kimya sio kweli” Alisistiza Mhe.
Nnauye.
Mhe.
Nnauye ameongeza kuwa watanzania wawe na desturi ya kutangaza mambo mema
yanayotokana na shindano hilo la urembo badala ya kutafuta mapungufu na
kuyakuza na yakaonekana kuwa ni tatizo kubwa katika machakato huo.
Aidha
amewahakikishia watanzania kuwa Miss Tanzania yuko salama na atashiriki vizuri
katika mashindano ya Miss World kwa mwaka 2016 watanzania wazidi kumwombea na
ikiwezekana kwa mwaka huu mrembo wa Dunia atokee Tanzania.
Katika
mashindano ya urembo kwa mwaka 2016 mrembo yaliyofanyika Jijini Mwanza na Bi Diana
Edward Luqumay alishinda taji hilo na anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano
ya Urembo ya Dunia 2016 yatakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu Washington Dc nchini
marekani na yatashirikisha nchi 119.

0 Comments