naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo akiagana na wanafunzi
wa shule ya sekondari msalato mara baada ya kuzungumza nao.
wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi selemani jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa
kidato cha nne unaofanyika Leo.
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali
mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne
unaoanza Leo nchini.
Katika ziara yake kwenye Shule ya
sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu
na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.
Akizungumza
na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani
huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia
mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha
chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.
Ameeleza
hatarajii mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka walimu wasisubutu
kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.
Jafo ame sema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.
Akizungumza
na wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa
vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.
Hata
hivyo amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga
kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka
kuwajibika ipasavyo.


0 Comments