Random Posts

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM.

 Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Maria Kullaya (kulia) akiwa ameambatana na Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi (kushoto) ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo wakiongea na mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke Dkt. Amani Malima.
 Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Msaidizi Maria Kullaya pamoja na afisa muuguzi wodi ya wazazi Bi. Agnes Mwampashe wakiwa wanaelekea katika wodi waliolazwa watoto njiti.
 moja ya wazazi waliopata kujifungua watoto njiti aliyeukutani ni Bi. Fausta Geson na wa kwanza ni Bi. Mariam Juma.

 Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Maria Kullaya kushoto akiwa ameambatana na Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi kulia wakimkabidhi zawadi mmoja ya wazazi aliyepata kujifungua mtoto njiti Bi. Fausta Geson.
Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwa katika picha ya pamoja hospitalini hapo. 

(Picha zote na Godfrey Peter)
........................................................................................................

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LIMEUNDWA KWA MUJIBU WA SHERIA NA LIPO KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA MBALIMBALI KWA JAMII, MAJUKUMU MAKUBWA YA JESHI NI KUZIMA MOTO NA KUOKOA MAISHA NA MALI. HIVYO BASI:-
KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI MAAFISA NA ASKARI (WANAWAKE) WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAMETEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE NA KUTOA ZAWADI MBALIMBALI KAULI MBIU IKIWI NI “OKOA MAISHA YA MTOTO NJITI”
KATIKA KUTAMBUA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI MAKUZI YA WATOTO HASA WANAOZALIWA KABLA YA WAKATI (WATOTO NJITI) MAAFISA NA ASKARI WANAWAKE WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAMEWAKADHI VIFAA MBALIMBALI KWA WAZAZI WALIOPATA KUJIFUNGUA WATOTO HAO NA WAZAZI WENGINE KUTOKANA NA WATOTO HAO KUHITAJI MAKUZI BORA NA VIFAA JOTO.

Post a Comment

0 Comments