Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mbaraka Yusup
bao la tatu leo kwenye mtanange wa VPL uliochezwa kwenye Uwanja wa
Kaitaba Mjini Bukoba. Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba
Kagera Sugar wamepanda juu nafasi ya Tatu kwenye Msimamo wa VPL baada
ya kuwanyuka bao 3-1 Timu ya Ruvu Shooting. Bao la kwanza la Kagera na
la kusawazisha limefungwa na Temi Felix kipindi cha pili baada ya
kuongeza kasi, Bao alilolifunga kwa shuti kali kwa mpira wa adhabu. Bao
la pili lilifungwa na Seleman Mangoma na la tatu likafungwa na Mbaraka
Yusuf. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Sehemu ya Benchi la Timu ya Kagera Sugar.
Mbaraka Yusuf alikunjuka zikiwa zimebaki dakika chache mpira
kumalizika na kumchambua beki wa Ruvu Shooting na kuziona nyavu za Ruvu
Rooting ambapo mpaka wakati huo Kipa hakuwepo langoni mwake. Ushindi huo
wa Kagera Sugar umewapandisha juu nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24.
Ligi hii ya Vodacom sasa inaenda mapumziko ya msimu wa kwanza wa
2016/2017.
Kipindi cha pili Tem Felix aliisawazishia bao Kagera Sugar na
Kisha baadae Seleman Mangoma akapachika bao la pili na kufanya Kagera
Sugar waongoze kwa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting.




0 Comments