Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima Bw. Godfrey Simbeye ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
TPSF akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya
Clarkson Insurance Brokers Justin Lambert mara baada ya uzinduzi wa
kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima Bw. Godfrey Simbeye ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF akizungumza wakati alipozindua Kampuni
ya bima ya Clarkson Insurance Brokers kwenye hoteli ya Hyyat
Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Tanzania Bw.Patrick Marimo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari .
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni
Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo akizungumza
kwenye uzinduzi wa kampuni ya Clarkson Insurance Brokers
inayojishughulisha na masuala ya bima, katika uzinduzi uliofanyika
mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini
Dar es salaam mwishoni mwa wiki
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers Justin Lambert akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat
Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni
Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo wa tano
kutoka kulia na Justin Lambert Mwenyekiti wa Kampuni ya Clarkson
wakikata keki kuashiria uzinduzi wa kampuni hiyo katika ofisi yao
iliyopoghorofa ya nane jengo la IPS Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam
kabla ya uzinduzi rasmi.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akizungumza na Balozi Mstaafu Peter Kalaghe wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akimsikiliza
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu
ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo wakati walipokuwa
wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa kampuni ya Clarkson Insurance
Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima, katika uzinduzi
uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro
Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Othman Chande akisalimiana na
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya JUNACO Group Of
Companies Limited ambayo ni Mwanahisa Mzawa Bw. Anic Kashasha wakati wa
uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Clarckson Insurance Brokers jijini Dar es
salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni
Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo
akiwatambulisha watendaji wa mbalimbali wa kampuni hiyo.
wageni waalikwa mbalimbali pamoja na wafanya kazi wa kampuni hiyo wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwanamuziki John Muhina kulia akiimba pamoja na wanamuziki wenzake wa bendi ya Tanzanite Band katika uzinduzi huo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
…………………………………………………………
Na Mwandishi wetu,
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)
imekaribisha uwekezaji zaidi kwenye sekta ya Bima nchini ili kuibua
ushindani utakaochochea ubunifu wenye tija zaidi kwa wadau wa sekta
hiyo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar
es Salaam, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni mpya ya Bima
ijulikanayo kama Clarkson Insurance Brokers Tanzania Limited,Mkurugenzi
Mtendaji wa TPSF , Bw. Godfrey Simbeye alisema ustawi wa uchumi wa nchi
kwa sasa unahitaji uimara na ubunifu zaidi kwenye sekta ya bima hivyo
wingi wa kampuni hizo unaweza kuwa na tija zaidi katika kufanikisha
hilo.
“Tanzania kwa sasa ipo kwenye
utekelezaji wa miradi mikubwa kama ile ya bomba la mafuta, ujenzi wa
reli ya kati, ujenzi wa barabara na majengo makubwa ya kisasa, vyote
hivi vinahitaji kulindwa na bima hivyo ujio wa kampuni kama hii ya
Clarkson Insurance Brokers Tanzania Limited tunauona kama ni heri na
wenye tija kwa taifa,’’ alibainisha.
Kwa mujibu wa Bw Simbeye kwa sasa
mchango wa sekta ya Bima kwenye Ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) ni chini
ya asilimia 1 huku akiitaja sekta binafsi kuwa ni miongoni mwa sekta
ambazo bado hazijafaidi ipasavyo matunda ya uwepo wa huduma za Bima
ambapo alitaja suala la ukosefu wa ubunifu miongoni mwa makampuni ya
Bima kuwa ni moja ya sababu ya uwepo wa changamoto hiyo.
“Matumaini yangu kwa kampuni ya Clarkson
Insurance Brokers Tanzania Limited kwa kiasi kikubwa yanachochewa na
ukongwe wao wa miaka 58 wakitoa huduma hii nchini Kenya ikiwa ni pamija
na Uganda hivyo natarajia kwamba uzoefu wao katika kipindi hicho kirefu
unaweza kuwa na tija zaidi hapa nchini,’’ aliongeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa makampuni
ya Bima ya Clarkson Insurance Brokers Tanzania Group Bw Justin Lambert
alisema pamoja na kutoa huduma kwa weledi, kampuni yake itajikita zaidi
katika kutoa elimu ya bima kwa jamii ili kuwavutia zaidi wengi ambao
kwasasa bado hawajaingia kwenye huduma hiyo.
“Clarkson Insurance Brokers hatujaingia
hapa nchini ili kuongeza idadi ya makampuni ya bima yaliyopo nchini bali
lengo letu hasa kuongeza ushindani na kuleta mapinduzi makubwa na yenye
tija kwa wadau wa sekta hii muhimu,’’ alibainisha.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
hiyo hapa nchini Bw, Patrick Marimo alisema mafanikio ya kampuni hiyo
katika soko lake jipya hapa nchini kwa kiasi kikubwa yatachochewa na
ubunifu mkubwa wa kampuni hiyo katika utoaji wa huduma zake.
“Tunalenga kuleta mabadiliko makubwa
kwenye huduma hii muhimu na ndio maana pamoja na mambo mengine
tutajikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii ili kuijengea uelewa zaidi
kwenye masuala ya bima ili tutoe huduma kwa watu wenye uelewa zaidi
…lakini pia uwekazaji wetu kwenye teknolojia ya kisasa unaweza kuwa
chachu zaidi katika kufikia malengo,’’ alisema.


















0 Comments