Mkuu
wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na Wananchi wa Pugu kinyawezi juu ya kuunda Timu ya watu wanne kutoka
miongoni mwa Wanachi waliokuwa na malalamiko watakaoungana na wataalam kutoka
Halmashauri na Ofisi yake kufuatilia malipo
na Fidia baada ya maelezo ya Mhandisi wa TAA kuwa majibu ya utata leo jijini
Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo na akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Wananchi walioshiriki kwenye
Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa,Awadhi Mtani katika Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua
maandalizi barabaraa Lumumba itakayo
tumika na Wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) kila siku ya Ijumaa, Jumamosi
na Jumapili. Leo jijini Dar es Salaam.akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg.
Msongela Palela, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni. na Katibu Tawala wa Wilala ya Ilala Edward Mpogolo
Mkuu
wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akisisitiza jambo mara baada ya kukagua maandalizi
ya barabara ya Lumumba kutumika na Wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) kila
siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili leo
(kushoto)ni ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi Ilala, Salum Hamduni.
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
..............................................................................................
Wananchi waliokuwa na maeneo/mashamba na nyumba katika eneo
la Pugu kinyawezi leo wamewasilisha malalamiko yao mbele ya Mhe. Sophia Mjema
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala.
Malalamiko hayo yanatokana na kuwepo kwa sintofahamu za hatma
ya maeneo yao ambayo yamechukuliwa na mamlaka ya uendelezaji wa viwanja vya
ndege. Wananchi hao kutoka katika Mitaa ya Kipunguni, Kigilagila na Kinyamwezi
hawajalipwa fidia kama ilivyokuwa imedaiwa kupitia mradi wa upimaji wa Viwanja
katika eneo hilo.
Wakizungumza katika Mkutano huo uliotishwa na Mkuu wa Wilaya
kwenye viwanja vya na kuhoji uhalali wa
mradi huo. Ofisi ya AfisaTarafa ya Ukonga ilielezwa kuwa, kuanzia mwaka 2001 hadi
2006 Mamlaka ya Viwanja vya ndege ilifanya uthmini wa maeneo mbalimbali ya
wenyeji wenye mashamba katika maeneo ya mitaa ya Kata za Pugu, Majohe na Mitaa ya Viwege, Kinyamwezi, Zavala, Mgeule
na Taliani.
Bw, Awadhi Mtani
akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Ramani za Mipaka za eneo mradi ambazo ni chanzo cha
mgogoro unaoendelea.
Hadi sasa ahadi zilizotolewa kuhusiana na malipo ya fidia
hayajafanyika na pia hawajapewa viwanja vyao na hali ikiwa mashamba yao
yamekwishachukuliwa. Sintofahamu hiyo imesababisha Wananchi wengi kukosa Imani
ya Serikali yao. Miongoni mwa wananchi hao wapo waliopokea fedha ambazo
hazilingani na thamani ya maeneo yao ambayo yameshachuliwa na pia hazitoshelezi
kumalizia ujenzi na kuwapelekea kuishi
kwenye nyumba za kupanga.
Mkuu wa wilaya
akisikiliza malalamiko ya wakazi wenye wenye malalamiko ya viwanja na nyumba
eneo la pugu kinyawezi
Aidha wakilalamika mbele ya Mhe. Sophia wananchi hao
wamewalaumu baadhi ya viongozi wanaosiamia mradi huo kwa kutowapatia taarifa
sahihi za mradi huo hali ambayo imesaabisha kuwepo kwa migogoro baina ya wakazi
hao hali inayotishia usalama wa Maisha miongoni mwao.
‘’Mhe Mkuu wa Wilaya
tunaomba kupewa viwanja vyetu’’ walidai wananchi hao
Akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Wilaya Bibi Gaudensia
Paskali alieleza kuwa wakati wa zoezi hilo nyumba zake tatu zilibomolewa na
alipofuatilia alipewa majibu ya kuwa kwakuwa nyumba zake ni za udongo hastahili
kulipwa fidia.
Aliendelea kueleza kuwa alifuatilia suala hili hadi kwa
aliyewahi kuwa WAZIRI WA Ardhi Anna Tibaijuka ambaye hakuwaki kukuonana naye hadi
leo hajafahamu hatma yake. Akiwa ni Mwanamke mjane hali hiyo imemsababishia
mgogoro na watoto wake wakimtuhumu kuuza eneo hilo.
Katika kubainisha mapungufu zaidi katika mradi huo baadhi ya
wananchi walilalamikia kupewa maeneo mbadala ambayo haiendani ya matumizi
yaliyokusudiw wapo waliopewa maeneo mbadala ambayo ni eneo la makaburi na siyo
makazi.
“Mheshimiwa Tunaishi
Maisha magumu, hatujui hatma yetu tunaomba utusaidie”
Mpima Ardhi wa Manispaa ya Ilala Bw. Ramadhani Chamwiti
akitoa ufafanuzi mbele ya Wananchi wa Mitaa ya Kipawa, Kigilagila na Kinyamwezi
katika Mkutano huo.
Mheshimiwa Mhe. Boniventure Mphuru Diwani wa Kata ya Pugu akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Wananchi walioshiriki kwenye
Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala uliofanyika leo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala aunda
Timu ya watu wanne kutoka miongoni mwa Wanachi waliokuwa na malalamiko
itakayoungana na wataalam kutoka Halmashauri
na Ofisi yake kufuatilia Majibu ya Wizara ya Ardhi kuhusiana na malipo ya Fidia baada ya maelezo
ya Mhandisi wa TAA kuwa na utata.





0 Comments