Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Kuelekea pambano la mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Timu ya Tanzania (Taifa
Stars) wanaotarajiwa kucheza na timu ya Taifa ya Zimbwabwe Kocha Mkuu wa
Charles Boniface Mkwasa kwa jina la utani Master ametaja kikosi ambacho
kinatarajia kuingia kambini Novemba 7,2016.
Mkwasa ametangaza majina hayo wakati
akizungumza na waandishi wa habari,amesema kuwa wataanza kambi hiyo kwa
ajili ya mchezo wao na Zimbwabwe na wachezaji wote wataungana na wengine
kuanzia Novemba 13 baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania
kumalizika.
“Mchezo wetu tunatarajia kucheza
ugenini mjini Harare Novemba 13 hivyo tunauchukulia umuhimu mkubwa kwetu
kutokana kuwa kwenye kalenda ya FIFA na sisi tunataka kushinda kutokana
na kushuka vibaya katika ubora wa viwango vya FIFA na kufika mpaka
nafasi ya 147 kitu ambacho ni hatari kwetu”alisema Mkwasa Wachezaji
wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Magolikipa:Aish Manura Azam,Said
Kipao JKT Ruvu na Deogratius Munishi
Mabeki:Erasto Nyoni, David Mwantika
wa Azam, Michael Aidan wa JKT Ruvu, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew wa
Yanga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba na James Josephat wa
Prisons.
Viungo:Himid Mao wa Azam , Mohammed
‘Mo’ Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamil Yassin wa Simba , wakati viungo wa
pembeni ni Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, Shizza Kichuya, Jamal
Mnyate wa Simba na Simon Msuva wa Yanga.
Watupia shavu: Ibrahim Hajib wa
Simba , John Bocco wa Azam FC, Elius Maguli timu ya Oman anacheza ,
Thomas Ulimwengu aliyemaliza mkataba wake TP Mazembe ya DRC , Omar
Mponda wa Ndanda na Mbwana Samatta wa K.R.C Genk ya Ubelgiji
0 Comments