Na.Alex Mthias.
Baada
ya kupokea kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Mbeya City hatimaye mabingwa
watetezi Yanga wameibuka na pointi tatu muhimu baada ya
kuwasambaratisha wenyeji Tanzania Prisons goli 1-0 mchezo wa Ligi Kuu
Tanzania bara kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mchezo
wa Leo ulikuwa mpira mkali kwa pande zote mbili huku timu zote
zikitumia mchezo wa kasi muda wote huku kosakosa ziliendelea kutawala
kutokana na ulinzi kuwa mzuri hadi mapumziko zilienda kupumzika zikiwa
hazijafungana
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya
mabadiliko kwa kumtoa kinda Yussuf Mhilu ambaye alianza na nafasi yake
kuchukuliwa na mchezaji bora wa mwezi wa Oktoba Simon Msuva na katika
dakika 54 Tanzania Prisons walikosa penati iliyopigwa na Lambert
Sabiyanka kuokolewa na kipa wa Zamani wa Prisons,Benno Kakolanya baada
ya Deus Kaseke kumchezea rafu Victoria Hangaya ndani ya kumi na nane.
Dakika
ya 74 Simon Msuva aliwanyanyuwa mashabiki wa Yanga ambao walifurika
uwanja wa Sokoine kuisapoti timu yao akiifungia timu yake kwa njia ya
mkwaju wa penati baada ya Obrey Chirwa kuchezewa rafu na beki wa Prisons
James Mwasote hilo likiwa goli la sita kwa Msuva msimu huu.
Kwa
matokeo hayo Yanga imefikisha pointi zao 30 katika nafasi ya pili
wakiwa wanazidiwa pointi tano na watani wao Simba ambao wameonja uchungu
wa kufungwa goli moja kwa bila na African Lyon na mchezo wa kufunga
mzunguko wa kwanza utamaliza siku ya Jumatano itakapovaana na Ruvu
Shooting kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Prisons:
Andrew
Ntala, Benjamin Asukile, Salum Kimenya, Leonsi Mutalemwa, James
Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambarti Sabiyanka, Mohemmed
Samata, Victor Hangaya/ Meshack Selemani dk82 na Jeremiah Juma/Salum
Bosco dk27
Kikosi cha Yanga:
Beno
Kakolanya, Mbuyu Twite, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan, Vicent Bossou,
Haruna Niyonzima, Thaban Kamusoko, Yussuf Mhilu/Simon Msuva dk46, Donald
Ngoma, Obrey Chirwa/Matheo Anthony dk90 na Deus Kaseke/Amissi Tambwe
dk56.
0 Comments