Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika eneo
ka Karen jijini Nairobi kwa ajili ya kufungua rasmi barabara ya kupunguza
msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji
wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa mara
baada ya kuwasili katika eneo la Karen jijini Nairobi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji
wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Rutto pamoja na
viongozi wengine, wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza
msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi
wa Karen nchini Kenya mara baada ya kufungua barabara ya Nairobi Southern
Bypass nchini Kenya.
Sehemu
ya barabara hiyo ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji
wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakicheza wimbo pamoja na kikundi cha kwaya
katika eneo la Karen mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Nairobi Southern
Bypass nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo
kutoka kwa Bi. Lucy Karuga kuhusu usindikaji wa mazao ya chakula katika kiwanda
cha Maziwa cha Eldoville katika eneo la Karen nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
usindikaji wa Samli katika kiwanda hicho cha maziwa cha Eldoville nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati
alipomtembelea nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo
na Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais Uhuru Kenyatta pamoja na Rais Uhuru
Kenyatta wakati alipomtembelea mama huyo
nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama
Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea
nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mama yake Rais Uhuru Kenyatta Mama Ngina
Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya. PICHA
NA IKULU















0 Comments