Random Posts

RAIS DKT. MAGUFULI AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI KENYA NA KUREJEA NYUMBANI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya kuondoka nchini Kenya na kurejea nyumbani Tanzania.
 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akimsindikiza mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuelekea kwenye ndege katika uwanja wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.
 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kabla ya kuondoka kurejea nyumbani nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mara baada ya kumaliza ziara yake  nchini Kenya.

 Picha na IKULU

Post a Comment

0 Comments