Random Posts

RAIS MAGUFULI NAPENDA MPIRA LAKINI SIYO SIMBA NA YANGA ZINAZONG'OA VITI BORA NIANGALIE NDONDO.

Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa kwa kweli yeye ni mshabiki mkubwa michezo na burudani lakini anashindwa kuhudhuria michezo kutokana na baadhi ya mashabiki wa timu fulani kufanya vurugu na mpaka kufikia hatua ya kung’oa viti uwanja wa Taifa.

DKT.Magufuli   ameyaongea hayo Leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali ambapo amesema kuwa anashwangazwa natua hiyo ya kufanya uharibifu mkubwa katika uwanja wa Taifa ambao ulijengwa kwa gharama kubwa tena ni kodi ya wananchi.

“Nasema kabisa bora nikaangalie mechi za ndondo kuliko kwenye kushuhudia mpira  wa Simba na Yanga wakati watu wanang’oa viti ambavyo havina hata makosa na hawajui gharama ya kuutengeneza huo uwanja”alisema Magufuli

Kwa kumbukumbu maneno ya Mh.Magufuli yanazilenga klabu kongwe hapa nchini Tanzania Simba na Yanga ambapo zilicheza Oktoba Mosi na mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 pamoja na kusababisha mashabiki kung’oa viti baada ya mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe kufunga goli ambalo liliaminika kuwa aliunawa mpira kabla ya kufunga na kumtoa nje kiungo Jonas Mkunde kwa kadi nyekundu hali iliyosababisha ghasia kwa mashabiki hao.


Aidha amesema kuwa hiyo ndio hali iliyosababisha kushindwa kujitokeza viwanja kushuhudia mechi mbalimbali hivyo yeye anapenda michezo toka moyoni mwake na pia amewaomba watu wenye tabia hiyo ya kufanya vurugu uwanjani waache mara moja.

Post a Comment

0 Comments