Mshehereshaji Luvanda akiwakaribisha wageni
wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya
StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw.
Leo Liao akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka
kampuni yake uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo akizungumza na wadau sekta ya Habari na
Mawasiliano wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni ya kidigitali kutoka
kampuni ya Startimes Tanzania uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es
Salaam.
Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes
Tanzania Bw. Juma Sharobaro akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya
kumpata mshindi wa moja ya televisheni za kidigitali katika hafla ya uzinduzi
wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw.
Leo Liao(kushoto) akikabidhi zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali yenye
upana wa inchi 40 kwa mshindi wa televisheni hiyo Bw.John Paul wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni
hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo(kushoto) akipokea zawadi ya moja ya
televisheni za kidigitali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw.
Leo Liao(kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika
Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo(kushoto) akikabidhi zawadi ya moja ya
televisheni za kidigitali yenye upana wa inchi 32 kwa mshindi wa televisheni
hiyo Bw.Ambokile Mapasa wakati wa hafla
ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es
Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo( wa
pili kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa kampuni ya
Startimes Tanzania jinsi ya televisheni za kidijitali zinavyofanya kazi wakati
wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao (kulia) akimueleza
jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo(kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa
televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba
16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Wasanii kutoka Dar es Salaam wakitoa
burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka
kampuni ya StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Na Mpiga picha Wetu.
..........................................................................................
Na
Mwandishi Wetu
Serikali
kupitia Wizara ya Ujezi Uchukuzi na Mawasilano imebariki uzinduzi wa
televisheni mpya ya kidigitali kutoka kampuni ya Startimes Tanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Prof Makame Mbarawa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Maria Sasabo amesema
Serikali imefarijika sana na ubunifu kutoka kwa kampuni ya StarTime Tanzania
kwa kuanzisha televisheni ya kidigitali isiyotumia kinga’muzi kupata matangazo
ya channeli mbalimbali.
“Hii
ni fursa kwa watanzania kujipatia televesheni hizi ambazo ziko katika teknolojia
ya hali juu sana ambazo zitasaidia Tanzania kuingia katika ulimwengu mpya wa
mapinduzi ya sekta ya Habari na Mawasiliano” alisema Bibi. Maria.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao amesema kuwa
StarTimes imelazimika kutoa televisheni hizo za kisasa ili kuendana na ukuaji
wa teknolojia ambapo wateja wataweza vipindi vinavyoenda na wakati katika ubora
wa hali ya juu.
“Tutahakikisha
tunawapa wateja wetu vipindi vyenye ubora na muonekano mzuri ambao wataufurahia
ulimwengu wa Digitali unaoendelea kubadilika kila kukicha duniani” alisistiza
Bw. Liao.
Ameongeza
kuwa televisheni hizo zimetengenezwa katika ubora unaotakiwa na ni rafiki kwa
mazingira na zimezingatia matumizi madogo ya umeme na zinapatikana kwa bei
nafuu ukilinganisha na televisheni kutoka makampuni mengine.
Televisheni
hizo za kidigitali zinaonesha zaidi ya channeli 100 za kitaifa na kimataifa
kuanzia habari, muziki, michezo, sinema, thamthilia,katuni, filamu na vipindi
vya Dini.










0 Comments