Mshambuliaji wsa Taifa Stars, Elius Maguri akichuana na beki wa
Zimbabwe, Hadebe Teenage katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe leo. Tanzania ilifungwa mabao
3-0.
Beki Michael Aidan wa Tanzania akijiandaa kumtoka mchezaji wa Zimbabwe, Danny Phiri katika mchezo huo.
..............................................................................................................
Na.Alex Mathias.
Timu
ya Tanzania 'Taifa Stars' imeshindwa kutamba ugenini dhidi ya wenyeji
Zimbabwe 'The warriors' baada ya kukubali kufungwa magoli 3-0 mchezo wa
kirafiki wa kimataifa uliochezwa uwanja wa Harare nchini Zimbabwe.
Dakika ya 7 Zimbabwe aliwapata goli la kwanza likifungwa na mshambuliaji hatari,Knowledge Musona anayecheza
klabu ya KV Oostende ya Ubelgiji baada ya mpira uliopigwa na Mathew
Rusike na Erasto Nyoni alishindwa kuokoa mpira huu na kumkuta mfungaji
katika sehemu nzuri ya kufunga.
Baada
ya kufungwa goli hilo vijana wa Mkwasa waliendelea kulisaka lango la
wenyeji na katika dakika 25 Samatta alikosa goli la wazi akiwa peke yake
na golikipa na dakika ya 27 Simon Msuva alioneshwa kadi ya njano baada
ya kujiagusha ndani ya 18 na kujindai kuwa kaangusha hadi mapumziko
wenyeji walikuwa mbele kwa goli hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji kuanza kulishambulia lango la Stars na mnomo dakika ya 54,Mathew Rusike alifunga
bonge la goli kwa shuti baada ya Musona kuukosa mpira na kumkuta
mfungaji akiwa na nafasi ya goli na kumchungulia Aisha Manula na
kumuacha akiwa hana la kufanya.
Alikuwa Musona tena dakika ya 56 alifunga goli la tatu kwa kichwa baada ya kupokea mpira toka kwa Willard Katsande ikumbukwe kuwa Knowledge Musona anacheza
Ligi moja na Samatta na katika klabu yake ya KV Oostende anaongoza kwa
ufungaji akiwa na magoli sita na timu yake inashika nafasi ya tatu
wakiwa na pointi 25 na msimamo wa wafungaji anashika nafasi ya nne.
Hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho Warriors
wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 3-0 na kwa matokeo hayo
yamewapa faida Wazimbabwe kuelekea katika viwango vya FIFA,kwa sasa
Zimbabwe wapo nafasi ya 110 katika ubora wa viwango vya FIFA na Tanzania
wamashika nafasi ya 144 na kwa kufungwa kwao kutawafanya washuke chini
zaidi wakati orodha itakapotolewa na FIFA.
0 Comments