Afisa wa jeshi la polisi kitengo cha
Usalama ,Haji Nduya akitoa mafunzo ya
usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es
Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kanda
maalum ya Dar es Salaam chini ya udhamini wa TBL Group, ikiwa
mkakati wa n kupunguza ajali za barabarani.
Mkaguzi
msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu
ya Jeshi hilo ,Erick ndidi (kulia) na Afisa wa Masuala Endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kushoto)wakitoa mafunzo ya
usalama barabarani kwa wanafunzi wa
shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam
Afisa masuala endelevu wa TBL Group
Irene Mutiganzi (kulia) akifafanua jambo kuhusiana na usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Oysterbay jijini ya Dar es salaam wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa
wanafunzi wa shule hiyo.
Wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi ya Oysterbay jijini Dar es
salaam wakionyeshwa alama za barabarani na
Afisa maswala endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kushoto) wakati wa mafunzo
hayo.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi
kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erickdidi akiongozana na wanafunzi wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar
es Salaam, kuvuka barabara ya Haile Selassie,
kwa kuongozwa na mwanafunzi wa shule hiyo Jesca John (kushoto) wakati wa
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Kanda maalum ya Dar es Salaam,yaliyodhaminiwa
na TBL Group ikiwa ni sehemu ya kupunguza ajali kwa watoto wa shule wakati
wanapovuka barabara wakienda au kutoka shuleni.
Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda
Walter akimkabidhi zawadi ya mkebe wenye vifaa vya shule mwanafunzi wa darasa
la kwanza katika shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jesca Reginald mara baada ya kujibu maswali yaliyohusu usalama
wa barabarani, wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Kanda maalum
ya Dar es Salaam,yaliyodhaminiwa na TBL Group ikiwa ni sehemu ya kupunguza ajali
kwa watoto wa shule wakati wanapovuka barabara wakienda au kutoka
shuleni.Kushoto ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama
barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi.
................................................................................................................................
Katika maadhimisho ya
Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki Jeshi
la Polisi Kanda ya mkoa wa Kinondoni liliendesha mafunzo ya usalama barabarani
katika shule ya msingi Oysterbay chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group.
Wakati wa mafunzo hayo
yaliyoendeshwa na askari kutoka Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani
wanafunzi waliweza kufundishwa alama
mbalimbali za bararani,mambo ya kuzingatia wanapokuwa barabarani na jinsi ya kuvuka barabara kwa tahadhari.
Pia wanafunzi walipata
fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na waliulizwa maswali ya chemsha bongo kuhusiana na elimu ya mafunzo waliyopatiwa.
Afisa mawasiliano wa TBL
Group,Amanda Walter, alisema kuwa TBL
imedhamini mafunzo haya ikiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za
serikali za kushirikiana na Jeshi la
Polisi katika kampeni za usalama
barabarani.
“Kampuni ya TBL tunao mkakati wa kuendelea kushirikiana na
serikali kupitia kikosi cha Polisi wa Usalama barabarani na wadau wengine
kuhakikisha tunapunguza matukio ya ajali za barabarani nchini ambazo zimekuwa
zikisababisha vifo,ulemavu na hasara kwenye jamii”.Alisema.
Alisema mpango wa
kuwafikishia wanafunzi wa shule za msingi elimu ya usalama barabarani hauna
budi kuungwa mkono kwa nguvu zote kwa
kuwa wakielewa tatizo hili mapema itakuwa ni rahisi kutokomeza tatizo hili
katika siku za usoni. “Wanafunzi wana uelewa mkubwa na ni
rahisi kushika wanayofundishwa pia wanaishi katika mazingira ambayo ni muhimu
kuwa na ufahamu wa masuala haya”.
Mbali na kudhamini
mafunzo haya ya wanafunzi kampuni ya TBL Group imekuwa mmoja wa wadhamini wakuu
wa Wiki ya Nenda Kwa Usalama ngazi ya kitaifa ambapo ilitoa vifaa mbalimbali
vya uhamasishaji ikiwemo gari maalumu ya kupimwa afya za madereva la Zahanati
inayotembea maarufu kama ‘Zahanati Mwendo’,huduma ambayo ni ya kwanza nay a aina
yake nchini ambayo mpaka sasa inaendelea
kuchangamkiwa na madereva popote linapopita gari hilo.






0 Comments