Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa
Uholanzi nchini, Jaap Frederiks (katikati) wakati Balozi huyo alipomtembelea
ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali
ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Kulia ni Eugene Gies ambaye ni Katibu
wa Uchumi na Sera za Biashara wa Ubalozi huo nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya alipokuwa anamfafanulia jambo Balozi wa
Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Alsuwaidi (kulia) alipomtembelea
Waziri Mwigulu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana
masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Balozi wa
Uholanzi nchini, Jaap Frederiks alipokuwa anamfafanulia jambo Waziri huyo
ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, walipokuwa wanajadiliana masuala
mbalimbali ua ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kulia ni Katibu wa Uchumi na Sera za
Biashara wa Ubalozi huo nchini, Eugene Gies.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto)akimsindikiza Balozi wa
Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Alsuwaidi mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es
Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa
Uholanzi nchini, Jaap Frederiks kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uholanzi na Tanzania. Mazungumzo hayo
yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.





0 Comments