Ngombe na mbuzi wakiwa wamesongamana chini ya mti pekee uliokuwepo
katika eneo lililopo karibu na Shule ya sekondari ya Oljoro mkoani
Arusha wakifuata kivuli ili kujikinga na jua Desemba 17, 2016.
Uharibifu wa mazingira unaosabishwa na shughuli za binadamu hasa
ukataji miti hovyo unaathiri hata viumbe wengine kama picha
inavyoonyesha.
Wananchi wakiwa wamebeba bango lenye maneno yanayoeleza suala la
uharibifu wa mazingira kuwa ni tatizo kwao katika mkutano uliohutubiwa
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye kijiji cha Ondenderet, Arusha
Desemba 17, 2016.
Mwendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda akiwa amejipumzisha
katika eneo lililoathiriwa na uharibifu wa mazingira unaofanywa na
binadamu katika kijiji cha Ormapinu, Arusha Desemba 17, 2016.
(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)



0 Comments