Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Viongozi wa Bandari ya Dar es salaam
mara baada ya kuwasili Bandarini hapo kwaajiri ya kufanya ziara.
.............................................................................................
NA EVELYN MKOKOI – DAR
ES SALAAM
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mzingira
Mhe. Luhaga Mpina amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es salaam
ili kujionea utaratibu wa Bandari hiyo wa kuondosha taka zitokanazo na shughuli
zake.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina imetokana na Malalamiko ya
wananchi yaliyodai kuwa uchafuzi mwingi umekuwa ukifanyika katika Bahari na
sehemu kubwa ya fukwe ya bandari imekuwa ikijaa taka za aina mbali mbali.
Kutokana na malalamiko hayo ya wakazi wa jiji la Dar es
Saalam, Naibu Waziri kabla ya kukagua maeneo ya kutoa na kukusanya taka za aina
mbali mbali katika bandari hiyo zikiwemo taka za mafuta ghafi, alipokea taarifa
kutoka kwa uongozi wa Bandari ambapo ameshangazwa na kile kilicholezwa na Afisa
Mazingira wa bandari Bwana Thobias Sonda kuwa Bandani hiyo kubwa katika kanda
ya Afrika Mashariki haina sehemu ya kupokea taka yaani waste reception facility na haina takwimu za taka zinazoingia na
kutoka Bandarini Hapo.
Akishindwa kujibu Baadhi ya Maswali yaliyoulizwa na Naibu
Waziri Mpina Afisa mazingira huyo alieleza kuwa, Bandari hiyo inazalisha aina
mbili kubwa za taka ikiwa ni taka za aina mbali mbali na taka za maji taka,
alisema kuwa taka hizo zinaondoshwa na wakala ambao wanasajiliwa na Sumatra lakini haikueleweka wazi kuwa,
taka hizo zinatupwa wapi na aliongeza kwa kusema kuwa, taka nyingi na hali ya
uchafu inayoonekana pembezoni mwa Bandari ya Dar es Salaam inatokana na
shughuli za kibinadamu kiwandani hapo, na kusema kuwa, kuna utaratibu wa
kufanya usafi na kuziondosha na kukanusha kuwepo kwa taarifa za boat na meli zinazofanya safari za
kuanzia bandarini hapo kuchafua mazingira ya bandari na Bahari.
Afisa Mazingira huyo, liongeza kwa kusema kuwa taka za maji
taka pamoja na kukosekana kwa takwimu za uondoshwani na umwagaji, zimekuwa
zikikuswanywa a magari yao maalumu na kumwagwa katika mabwawa yao yaliyopo
Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kwa kushangwazwa na hali hiyo, Mpina kupitia Baraza la taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC ameutaka uongozi wa Bandari hiyo
kujenga mfumo mzuri wa kuhifadhi taka kwa muda wa miezi sita na kuripoti kwa
Baraza za Mazingira kwa miezi mitatu Mfulizo kuonyesha namna ambavyo uondoshaji
wa taka hizo unafanyika, Pamoja na kuwasilisha ripoti kwa Baraza ya Namna ambavyo mawakala hao walipatikana.
Aidha Naibu waziri Mpina ameliagiza baraza kumpelekea
ripoti ndani ya siku saba, inayoonyesha
kama hao mawakala wa kukusanya taka bandarini wapo kisheria.
Kwa Upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Nchini Bw.
Nelson Mlele amesema kuwa amepokea maagizo ya Mhe kupitia NEMC kwani
yanawakumbusha utekelezaji wa majukumu yao na kwa upande wa Bandari ni
changamoto itakayofanyiwa kazi haraka.;

0 Comments