Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa
Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer (kulia), akikabidhi mfano wa hundi
yenye thamani ya shilingi 48,064,958 kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Ereto East Africa
Foundation Mch. Godsave Ole Megiroo (kushoto),
ikiwa ni msaada wa fedha zilizotolewa na benki hiyo kusaidia
uboreshaji wa mazingira ya shule ya Mairowa Integrity katika ujenzi wa
vyoo na eneo la kufulia. Wapili kushoto ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa
shule
ya Mairowa Integrity Bi. Elizabeth Mollel na mwalimu wa shule hiyo
BiNancy Mseli (watatu
kushoto).
Meneja
wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer
(kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani)
wakati wa hafla ya makabidhiano ya Shilingi Milioni 48,064,958
kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation. Katikati ni Mwalimu Mkuu
Msaidizi wa shule ya Mairowa Integrity Bi. Elizabeth Mollel na mwalimu wa shule hiyo Bi Nancy
Mseli.
Meneja
wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer
(kulia), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamni ya shilingi 48,064,958 kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Mch. Godsave Ole Megiroo (kushoto). Pamoja nao kwenye picha ni wafanyakazi wa benki ya KCB Tawi la TFA, Arusha.
Afisa Biashara wa benki ya KCB Tawi la TFA, Arusha, Amedeus Tumaini akitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya
makabidhiano ya Shilingi Milioni 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation.
....................................................................................................................
Dar es Salaam, 19 December, 2016 – Benki ya KCB Tanzania imekabidhi rasmi mchango wa shilingi 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation ikiwa ni mwitiko kwa ombi la Taasisi hiyo kwa ajili ya
ujenzi wa vyoo 16 vya kuflashi na eneo la kufulia katika shule ya Mairowa Integrity
iliyo chini ya uongozi wa taasisi hiyo.
Benki ya KCB ilikua imeshawasilisha
mchango huo tokea mwezi wa tatu mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla
ya makabidhiano, Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB, Hogla
Laizer alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika
uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.
“Benki ya KCB Tanzania inadhamini
uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya
vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni
kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Bi. Laizer alisema na kubainisha kwamba
tangu ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa ikijikita
katika kuisadia jamii.
Akitolea mfano wa michango
iliyotolewa na benki hiyo katika kuboresha huduma za elimu nchini, Bi.
Lazier alisema: “Kupitia miradi hiyo benki ya KCB Tanzania imeshatumia shilingi
milioni miatatu kusaidia shule zaidi ya 20 kwa kuzipatia
madawati pamoja na vifaa vingine vya kuboresha huduma na mazingira ya
shule.”
Alimaliza kwa kusema benki ya KCB ina kawaida ya kutembelea shule zote ambazo imepeleka
misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kuona manufaa yanayotokana na msaada
husika. Hivyo aliieleza taasisi hiyo kuwa matunzo na matumizi mazuri ya mchango
uliotolewa, ndo itaifanya benki ya KCB iongeze msaada katika shule ya Mairowa Integrity iliyo chini ya
uongozi wa Ereto East Africa Foundation.




0 Comments