Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla katikati akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa
kutoa maagizo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali juu ya kufuatilia vilainishi .
Kushoto kwake ni Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele na
kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Dk. Mohammed Ali .
PIcha Na Ally Daud-MAELEZO
..................................................................................................................................
Na Ally Daud MAELEZO Dar es Salaam.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Mkemia
Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele kuendelea na uchunguzi wa
kimaabara kwa vilainishi vilivyo sokoni ili kubaini bidhaa isiyokidhi
viwango.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Jijini Dar es Salaam wake na Dkt. Kigwangalla amesema Ofisi ya Mkemia Mkuu
wa Serikali haina budi kuendeleza uchunguzi wa kimaabara ili kubaini vilainishi
visivyo na viwango na ubora ambavyo vinaendelea kutumiwa.
“Tunapiga marufuku uuzaji wa
vilainishi vya kupima unaofanyika mtaani na sokoni kwa sababu vifungashio vya
vilainishi hivyo havikidhi ubora” alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha Dkt. Kigwangalla amesema Serikali
itaendelea kupiga marufuku kuingizwa kwa vilainishi vilivyotumika (recycled
lubricants) visivyo na ubora na visivyo kidhi matakwa ya kisheria kwani vinachangia
uharibifu wa vyombo vya moto nchini.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla
amesema kuwa asilimia 50 ya vilainishi vya injini, aina ya petroli
zilizochunguzwa zilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya
kitaifa.
Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa
Serikali, Prof. Samwel Manyele amesema kuwa amepokea agizo la
Naibu Waziri na amesema kuwa uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za
vilainishi zinazoingizwa nchini unafanyika na kuendelea.
Aidha Prof. Manyele amesema kuwa
mpaka sasa wamesajili kampuni 28 za kuingiza vilainishi nchini na
wameimarisha ukaguzi wa mizigo ya vilainishi katika
viwanda, bandari, bandari kavu, mipaka na viwanja vya ndege.
Kwa mujibu wa Prof. Manyele amesema
kuwa miongoni mwa vilainishi hivyo vinavyoingia nchini ni pamoja na mafuta ya
kulainishia injini ,Diseli na Petroli

0 Comments