Random Posts

DSTV WASHEHENISHA KAPU LA SIKUKUU KWA VING’AMUZI VYA BURE!

 Decemba 23, 2016.           
Katika kusheherekea msimu huu wa krismasi Multichoice Tanzania Kupitia King’amuzi chake maarufu cha DStv imemwaga zawadi ya ving’amuzi vya kisasa vipatavyo 24 pamoja na vifurushi vya mwezi mzima kwa washindi wa shindano la ‘Kapu la Sikukuu’ lililoendeshwa kwa ushirikiano na kituo cha redio cha EFM.
 Washindi hao sasa wataweza kusherehekea kwa mbwembwe sikukuu ya krismass na mwaka mpya huku wakiangalia chaneli zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (laLiga) na ligi ya Uingereza. Pia katika kifurushi hicho wanachopata kama zawadi kina chaneli ya Maisha Magic Bongo yenye simema na tamthilia za kitanzania ikiwemo Tamthilia maarufu ya HUBA ambapo wakongwe wa filamu nchini kama Muhogo Mchungu, Riyama Ali, Mboto na  Hashim Kambi wanaonekana kwenye tamthilia hiyo iliyojitwalia umaarufu mkubwa.
 Katika kunogesha hafla hiyo, Waigizaji maarufu nchini “Mboto” na “Irene Paul” ndiyo waliokabidhi zawadi kwa washindi katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema jana.
Akizungumza muda mfupi kabla ya washindi hao kukabidhiwa zawadi zao, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria alisema kampuni yao imeamua kuwatunuku washindi hao ving’amuzi na vifurushi vya mwezi mzima vya DStv ili kuwafanya wao na familia zao kusherehekea krismass na mwaka mpya kwa mbwembwe na bashasha majumbani kwao huku wakitazama DStv.
Amesema kuwa Multichoice Tanzania hawajawatunuku washindi wa Kapu la sikukuu tu, bali watanzania wote kwani hivi karibuni walishusha bei za virfurushi vyao kwa wastani wa asilimia 16, huku kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi Shilingi 19,975 tu!
Kwa mawasiliano zaidi:

Instagram (@DStvTanzania), Twitter (@DStv_TZ), Facebook (@DStvTanzania) and website (www.dstv.com)

Post a Comment

0 Comments