Kaimu Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake fupi ya kufunga mwaka
2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017 kwenye Baraza la Maafisa na Askari kutoka
vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Dar es Salam Desemba 30, 2016 katika Bwalo
Kuu la Maafisa Magereza Ukonga.
Naibu
Kamishna wa Magereza, Edith Mallya akimkaribisha Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt.
Juma Malewa(katikati aliyeketi) kabla ya kuongea na Maafisa na Askari wa Jeshi
la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na
kuukaribisha mwaka mpya 2017(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa D ar es
Salaam, SACP. Augustine Mboje. Baraza hilo limefanyika Bwalo Kuu la Maafisa
Magereza Ukonga, Dar es Salaam Desemba 30, 2016.
Kaimu Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akijibu kero mbalimbali zilizoulizwa na
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam(hawapo pichani)
katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017
Askari
wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza ya Mkoa wa Dar es
Salaam wakisikiliza hotuba ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt.
Juma Malewa(hayupo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na
kuukaribisha mwaka mpya 2017.
Afisa
Utumishi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu wa Magereza Elmas Mgimwa akitolea
ufafanuzi kuhusiana na masuala ya kiutumishi yaliyoulizwa na Maafisa na Askari
wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam(hawapo pichani) katika Baraza hilo.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mkubwa
hotuba ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kwenye
Baraza hilo.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).






0 Comments