Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. William Lukuvi akipokelewa kwa maandamano na mabango na mamia ya wananchi
wa kata ya Nyarubanda katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma ambao kwa muda
mrefu wamekuwa na kero ya ardhi baada ya mmoja wa wakazi wa kijiji hicho
kujimilikisha eneo la serikali ya kijiji.
Wakazi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakiwa
na nyaraka za migogoro ya ardhi walizo zileta ili kumpatia Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi aweze kuitatua migogoro yao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. William Lukuvi akitatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa Kasulu mara baada ya
kupokea malalamiko hayo.
Wakazi wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wenye
migogoro ya ardhi wakimsikiliza Mh. William Lukuvi wakati akitatua migogoro yao
ya ardhi.





0 Comments