Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Lukuvi akiwapatia hati miliki za Ardhi kwa jamii ya wa Hadzabe
wanaoishi wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Wa Hadzabe wakimkaribisha Waziri wa ardhi,Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kwa kumvusha taji.
Wa Hadzabe wakifurahi na Waziri wa ardhi,Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi baada ya kuwapa hati miliki za Ardhi.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Lukuvi (wa nne kulia mbele) akiwasili wilayani Karatu kwa ajili ya
kuwapatia hati miliki za Ardhi jamii ya wa Hadzabe.
Wakazi wa kijiji cha Midabini wilayani Karatu
Mkoani Arusha wakisimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero zao za
ardhi, ambapo Waziri Lukuvi alisimama na kuzitatua.
Wakazi wa kijiji cha Mang’ola juu wilayani
Karatu Mkoani Arusha waliosimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi wakimsikiliza wakati
akitatua mgogoro wao wa Ardhi.
.............................................................................................................................
Na Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Lukuvi amewapatia hati miliki za Ardhi kwa jamii ya wa Hadzabe wanaoishi
wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri Lukuvi amefika katika maeneo yao na kuwapa hati
miliki za kimila kwa vijiji na wanayoishi jamii ya wa Hadzabe na jamii nyingine
za kifugaji ili kulinda maeneo yao ya malisho na maeneo wanayotumia kuwinda
wanyama.
Jamii ya wa Hadzabe ni watu ambao huishi kwa mfumo wa maisha
ya kuwinda, kufuga wanyama pori na kula mimea na matunda ya miti
inayowazunguka. Jamii hii kwa miaka mingi imekuwa ikiishi bila kufuata mipaka
ya maeneo yao na hivyo kusababisha migogoro ya ardhi kwa jamii nyingine
zinazoishi karibu na maeneo yao.
Pamoja na ziara hiyo Mhe. William Lukuvi amtatua migogoro ya
Ardhi ya wananchi wa wilayani Karatu Mkoani Arusha na wananchi walio na kero za
migogoro ya ardhi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kupokea vielelezo vya kero za
wananchi walizoziwasilisha kwa Waziri ili azitolee maamuzi.
Wananchi wa vijiji vya Mang’ola juu na Midabini wilayani
Karatu Mkoani Arusha walisimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero
zao za ardhi, ambapo Waziri Lukuvi alisimama na kuzitatua pamoja na kumuagiza
Mkuu wa wilaya ya karatu Bibi Therezia Mahongo kutafutia ufumbuzi baadhi ya
migogoro hiyo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo
imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya
Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desemba
ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma
mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu
na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani
Chato.
Pia Mhe. Lukuvi ametatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Mara
katika wilaya za Musoma na Bunda ambapo kwa Arusha ametatua migogoro ya wilaya
ya Arumeru na Karatu.
0 Comments